MASHINDANO ya kuogelea ya
Taifa ya umri mdogo yamepangwa kuanza leo nchini Kenya ,
huku Tanzania
ikipeleka waogeleaji 25.
Mashindano hayo ya siku tatu
yamepangwa kufanyika katika bwawa la shule ya Aga Khan nchini humo na
kushirikisha waongeleaji 2000 kutoka ukanda huu wa Afrika.
Katibu msaidizi wa Chama cha
Kuogelea nchini TSA, Ramadhan Namkovela amesema kuwa mashindano hayo
yanashirikisha vijana wenye umri wa miaka 11 kushuka chini.
Alisema kuwa Tanzania
imepeleka waogeleaji wenye umri wa miaka 7 hadi 11, ambapo michuano hiyo
itasaidia kukuza viwango vya waogeleaji hao.
Aliwataja waogeleaji hao kuwa
ni Reuben Monyo, Njukia Kihara, Prashraad Magesvaran, Oliver McIntosh, Shiv
Shreekumar, Gian Maria, Vansh Ladwa, Dhashraad Magesvaran, Alexander Belikov,
Harry McIntosh, Urav Shah, Maia Tumiotto, Diya Patel, Amani Doggart.
Wengine ni Celina Itatiro,
Tessa Francis, Janice Njuguna, Smriti Gokarn, Selina Mehta, Sonia Tumiotto,
Maya Kihara, Mariana Pipollo, Piya Shah, Talin Stengel and Ursula Khimji.
Mkuu wa Msafara Inviolata
Rwelamira-Itatiro, Kocha Mohamed Abdulaziz, Kocha Alex Mwaipasi, Kocha Kanis
Mabena.
No comments:
Post a Comment