Mario Gotze |
MUNICH, Ujerumani
UMESIKIA? Mario Gotze aliumia katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baina ya Borussia Dortmund na Real Madrid, iliyofanyika Santiago Bernabeu na kwamba kuna hofu kubwa kwamba akakosa mechi ya fainali ya michuano hiyo itakayofanyika Jumamosi ijayo, Wembley Stadium.
Kwa mujibu wa Juergen Klopp (alichokisema kupitia Bundesliga.com), nyota wake huyo No. 10 ameanza kufanya mazoezi ya kukimbia na pengine anaweza akapangwa kwenye mchezo huo.
Wasiwasi mkubwa umekuwa juu ya hali ya Gotze na kama atakuwa fiti kuweza kucheza mchezo huo, kitu ambacho hadi sasa hakieleweki. Gotze ni mchezaji ambaye anaweza kubadili sura ya mchezo, pindi mpira unapokuwa kwenye miguu yake.
Lakini, ukweli ni kwamba kutakuwa na hofu zaidi katika kikosi hicho kama itamkosa Marco Reus. Bila ya kufanya mzaha hapa, Reus ni mchezaji ambaye hakika atakuwa mtihani mgumu kwa Bayern.
Mbinu za ufundishaji za Jupp Heynckes zinafanana na zile za Arrigo Sacchi, kutumia zaidi kutegea 'offside', kitu ambacho kama Dortmund watamtumia Reus itakuwa kazi ngumu kwa Bayern.
Bayern ni timu inayocheza kwa tahadhari kwenye safu yake ya ulinzi. Walipocheza dhidi ya Barcelona, waliweza kulinda nyavu zake zisiguswe kwenye uwanja wao wa Allianz Arena na hata walipokwenda Camp Nou.
Kabla hawajawafunga Juventus jumla ya mabao 4-0 kirahisi kabisa, walimzima Andrea Pirlo na wakaweza kuyatuliza mashambulizi yote ya Bianconeri.
Kulinda nyavu zao zisiguswe walipocheza ya washambuliaji wakali kama Lionel Messi, Mirko Vucinic na David Villa, jambo hilo litawatia hofu mashabiki wa BVB, na kwamba mjadala uliopo kwa sasa kama Robert Lewandowski ataweza kuibomoa ngome hiyo au la.
Na jambo hilo litabaki kusubiri kufanywa na mtu 'genius' na Reus ana kila kiwango kinachomfanya awe na uhakika wa kulifanya hilo. Ni mchezaji mahiri zaidi kwa kupiga pasi, lakini ubora unaomfanya atishe zaidi ni uwezo wake wa kukokota mipira na kufyatuka mashuti kitu ambacho kinamfanya awe mchezaji anayevutia kutazama.
Amekuwa akifunga mabao mengi sana ya aina hiyo, akiwa kwenye kasi na amekuwa na uwezo pia wa kupangua ngome ya wapinzani kwa kadri anavyotaka.
Akiwa mchezaji mwenye ubora usio na shaka kama alivyo Goetze, Reus nafasi yake ya kutofikiriwa sana ndani ya uwanja, ndicho kitu kinachomfanya apate nafasi ya kuwaduwaza wapinzani wake na kasi yake ni kitu ambacho kimekuwa kikiwatesa mabeki wengi wa timu pinzani.
Marco Reus |
Javi Martinez atakuwa na kazi hiyo rasmi na ni wazi kabisa atapaswa kucheza kwenye nafasi yake kwa nidhamu kubwa kabisa, wakati patna wake katika sehemu hiyo ya ulinzi, Dante anamaliza matatizo mengine ambayo yanaweza kuibua matatizo kutoka kwa Dortmund.
Kama Reus atapata muda wa kutawala mchezo huo, kuna nafasi kubwa ya Dortmund kushinda mchezo huo wa fainali na hatimaye kunyakua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya msimu huu.
No comments:
Post a Comment