MARA ya kwanza aliingia kwenye uwanja wa soka akiwa kama winga asiyefahamika kabisa, akitumia zaidi mguu wa kulia, kitu ambacho kilimfanya kuwa silaha ya maangamizi ya Manchester United.
Na sasa anaondoka akiwa mwanamichezo maarufu duniani, tajiri kwenye mchezo huo wa soka na mtu ambaye atabaki kuwa katika kumbukumbu ya milele ya mchezo wa soka, hasa kwa kile alichokifanya kwa nyakati tofauti katika mchezo huo.
Huyu si mwingine, ni David Beckham. Uamuzi wake wa kustaafu soka si kwamba umekuja kwa dharura mno na kuwashangaza wengi, hapana.
Anatimiza miaka 38 na amecheza mechi chache sana tangu alipojiunga kwa mkataba mfupi kwenye klabu ya Paris Saint-Germain Januari mwaka huu, sawa nahodha huyo wa zamani wa England, angeweza kuendelea walau kwa mwaka mmoja, lakini ameamua kumaliza soka akiwa na hadhi yake.
Wikiendi iliyopita, alisherehekea PSG kutwaa taji lao la Ligue 1, walilotwaa kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri kwa miaka 19 na kwa namna moja au nyingine, mchezaji huyo alishiriki kwa kiasi fulani katika ubingwa huo.
Mwakani alitambua wazi kabisa anafahamu kwamba, asingeweza kuwa katika hali aliyonayo kwa sasa. Kutokana na klabu anayochezea kuwa na fedha nyingi na kufikiria kuimarisha timu yao kwa kufanya usajili mkubwa mwishoni mwa msimu huu, nafasi yake ya kupata nafasi ya kuichezea timu hiyo ingekuwa finyu. Hivyo uamuzi wa kustaafu soka ameufanya katika kipindi mwafaka.
Lakini, kuondoka kwake kutalifanya soka kuwa masikini kidogo. Beckham wakati anaanza kucheza soka la kulipwa katika kikosi cha kwanza, ndicho kipindi kinachoaminika kwamba kilikuwa cha michezo kutawala kwenye televisheni.
Taji la Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya yote hayo yalianza sawa na Beckham, katika msimu wa 1992-93, ambapo dunia ya mchezo huo ilipoanza kubainisha utajiri mkubwa kwenye mchezo huo.
Wakati alipoanza kupata uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza, aliweza kufanya kitu ambacho wazi kilitambulisha kipaji chake na mwonekano wake ambao ulivutia dili nyingi za udhamini.
Wakati alipokutana na kuoana na binti wa kundi la Spice Girl, alipata umaarufu mkubwa kutokana na kuwa na Victoria, lakini Beckham alitafuta namna nyingine ya kuweza kuandikwa kwenye magazeti kwa mambo yake mwenyewe.
Akiwakilisha England kwenye fainali za Kombe la Dunia 1998, likaja suala la Simeone, nyota wa Argentina, likamtibua sana na kumsababishia mambo mengi, lakini akavuka kikwazo hicho akiwa kama moja ya wachezaji waliotoka kwenye kizazi cha dhahabu cha Man United, mpira wake wa adhabu aliopiga kwenye mechi dhidi ya Ugiriki, ilianzisha zama mpya kwa Beckham.
Kwenye kikosi cha United, aliweza kutwaa mataji chini ya kocha wake Sir Alex Ferguson, kabla ya mahusiano yake na bosi huyo kuingia kwenye mtafaruku kidogo.
Kitendo cha kupigwa na kiatu na Ferguson kilichochea mpango wa kuihama timu hiyo na akaenda kutua Real Madrid kwa ada pauni milioni 35, uhamisho ambao uliokuwa na thamani kubwa Bernabeu kuliko zama zote za ‘Galactico’.
Licha ya kuwa na matatizo na Fabio Capello, baada ya kutangaza kwamba anakwenda Hollywood, Beckham muda wake aliokuwa na miamba hiyo ya Hispania, haukumalizika patupu, kwani aliweza kutwaa ubingwa wa La Liga na kuboresha rekodi zake katika mchezo huo.
Steve McClaren uamuzi wake wa kumweka kando Beckham kwenye soka la kimataifa, aliofanya kwa haraka mno na alionekana kama alimtazama mchezaji huyo katika jicho la wasiwasi.
Beckham aliweza kurejea kwenye kikosi ndani ya mwaka mmoja na kuweza kuandika rekodi yake ya kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika kikosi cha England.
Pengine hakuwezi kutwaa taji lolote na timu yake ya taifa, lakini kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia mara mbili na nane bora ya michuano ya Euro 2004, kwa upande wa Beckham alijitolea kwa kila kitu katika jezi hizo.
Alipokwenda LA Galaxy, wengi waliamini kwamba alikwenda kujimaliza kabisa, lakini mahali hapo bado aliendelea kucheza kwa kiwango kikubwa na kupata nafasi ya kujiunga kwa mkono mara mbili katika kikosi cha AC Milan na hivyo alizidi kujihakikishia namba katika kikosi cha Capello.
Akiwa na timu hiyo ya Marekani, aliweza kutwaa mataji mawili ya MLS, kabla ya kutua PSG na kutwaa Ligue 1 katika msimu wake wa kwanza tu.
Mafanikio yote hayo kwa Beckham hayakuweza kutimiza furaha yake kama tu atakosa nafasi ya kuchezea timu ya taifa. Nchini Marekani alicheza kwa kiwango kikubwa, lakini hilo haliwezi kumpa furaha yake kwasababu tu ya kukosa kucheza timu ya taifa.
Kiukweli, Beckham ataendelea kukumbukwa na kile alichokuwa akikifanya ndani ya uwanja na nje ya uwanja, lakini wanasoka wote wa kizazi cha sasa daima watampongeza kutokana na namna alivyotumia fursa iliyopo kutangaza kipaji chake. Kwa Beckham, siku zote soka kilikuwa kitu cha kwanza.
No comments:
Post a Comment