MABINGWA Manchester United
leo walitua Emirates kuchezea Mechi yao ya kwanza tangu wanyakue Ubingwa wa BPL,
Barclays Premier League, na walipokelewa na Wachezaji wa Arsenal kwa Gwaride la
Heshima kabla Mechi kuanza ikiwa pia ni Mechi ya kwanza kwa Nahodha wao zamani,
Robin van Persie, kurudi Uwanjani hapo tangu awahame, Mechi ambayo ilimalizika
kwa Bao 1-1 huku Van Persie akiifungia Man United bila kushangilia Bao lake.



Robin van Persie alifunga kwa Penati katika Mechi yake ya kwanza kucheza Uwanja wa Emirates tangu ahamie Man United kutoka Arsenal mwanzoni mwa Msimu huu katika Mechi ambayo ilimalizika sare ya Bao 1-1 matokeo ambayo si mazuri kwa Arsenal katika mapigano yao kufuzu katika 4 Bora kwani mapema Chelsea waliifunga Swansea na kuwapiku nafasi ya 3.

Pia Tottenham wako nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal lakini wana Mechi mkononi.

Arsenal ndio walitangulia kufunga katika Mechi hii katika Dakika ya pili baada ya pasi ya kutanguliziwa kumkuta Theo Walcott akiwa Ofsaidi ya wazi na kufunga Bao ambalo lilisimama kama lilivyo.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 44 kwa Penati iliyolewa na Refa Phil Dowd baada ya Bacary Sagna kumchezea Rafu Robin van Persie ambae yeye mwenyewe alifunga Penati hiyo bila kushangilia ikiwa ni heshima kwa Klabu yake ya zamani.
Hilo ni Bao la 25 kwa Van Persie katika BPL likimfanya aongoze kuwa Mfungaji Bora akifuatiwa na Luis Suarez mwenye Bao 23.
















Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Rosicky (Wilshere 62), Arteta, Walcott, Ramsey (Oxlade-Chamberlain 78), Cazorla, Podolski (Gervinho 71)
Subs not used: Mannone, Vermaelen, Monreal, Jenkinson
Booked: Sagna, Walcott, Oxlade-Chamberlain
Goal: Walcott 2
Manchester United: De Gea, Rafael (Anderson 73), Evra, Jones, Ferdinand, Evans, Valencia, Carrick, Nani (Giggs 83), Rooney (Hernandez 87), Van Persie
Subs not used: Lindegaard, Buttner, Cleverley, Kagawa
Booked: Rafael, Jones, Van Persie, Evans, Valencia
Goal: Van Persie 44 pen
Referee: Phil Dowd
Attendance: 60,112
No comments:
Post a Comment