KOCHA Mkuu
wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic na kiungo wa timu hiyo, Haruna Moshi
‘Boban’ wametajwa kuiua Simba, baada ya kutimuliwa katika mzunguko wa pili wa
Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza
na jijini jana, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Abdallah ‘King’ Kibadeni, alisema
uongozi wa klabu hiyo, ulifanya makosa makubwa ya kuwatimua nyota watatu wa
timu hiyo, ambao ni Boban na mabeki wao,
Amir Maftah na Juma Nyosso.
Kibadeni
alisema kilichosababisha Simba ishindwe kutetea ubingwa wao, ni kuwatimua
wachezaji hao na kocha wao katikati ya msimu kitu ambacho kiliathiri mfumo
mzima wa uchezaji.
Alisema
katika mzunguko wa kwanza, Simba ilianza vizuri lakini ilipoteana baadaye baada
ya uongozi wa klabu hiyo kubadilisha benchi la ufundi, ambalo lilichukuliwa na
Kocha, Patrick Liewig akisaidiana na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.
Kibadeni
alisema uongozi wa Simba usingefikia uamuzi wa kumtimua Milovan, pamoja na
mgawanyiko ambao umetokea kati yao na wanachama wa tawi la Mpira Pesa kuhusu
matokeo mabaya ya ligi hiyo.
“Hakuna mtu
wa nje aliyeivurunga Simba, bali ni watu waliopo ndani ya klabu hiyo
waliyoivuruga timu hiyo, jambo lingine ni pale kumtimua Milovan tayari
alishaandaa kikosi chake na wachezaji waliozoea mfumo wake,” alisema Kibadeni.
Alisema Liewig
asingeweza kupata mafanikio ya muda mfupi baada ya kukabidhiwa timu hiyo
kutokana na mfumo wake wa ufundishaji.
Kibadeni alisema suala la kuachwa kwa
wachezaji wakubwa na kupewa nafasi vijana pekee, hali hiyo ilichangia Simba
kuwa na matumaini madogo ya kuibuka na ushindi katika mechi zao.
Simba kwa
sasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo, huku Yanga ikiwa
imechukua ubingwa baada ya kufikisha pointi 56 ambazo hazitafikiwa na timu nyingine.
No comments:
Post a Comment