Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, April 14, 2013

MANCHESTER CITY YAIFUNGA CHELSEA 2-1 SASA KUCHEZA NUSU FAINALI NA WIGAN ATHLETICS KWENYE FA CUP JUMAMOSI

Manchester City leo wamejipa matumaini ya angalau kutwaa Kombe moja Msimu huu kwa kuwabwaga nje Mabingwa watetezi wa FA CUP Chelsea kwa kuwapiga Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali iliyochezwa Uwanjani Wembley na wao kutinga Fainali ambapo watacheza na Wigan Ahletics.
Man City, ambao wapo nyuma ya Man United kwa Pointi 15 katika BPL, Barclays Premier League, wakiwa wamebakiza Mechi 7 na Man United wamebakiza Mechi 6 huku wakihitaji Pointi 7 kati ya hizo kutwaa Ubingwa, tayari, kama alivyokiri Meneja wao Roberto Mancini, wasalimu amri kutetea Taji lao la Ubingwa wa BPL.
Kwa Wadau wengi hii ni nafasi murua kwa Man City kutwaa Taji na hii itakuwa ni mara ya pili katika Misimu mitatu chini ya Roberto Mancini kutwaa FA CUP kwani walibeba Kombe hili katika Msimu wa kwanza wa Mancini wa 2010/11.

Kwa Chelsea, chini ya Meneja wa muda Rafael Benitez, nafasi pekee ya wao kutwaa Taji Msimu huu ni EUROPA LIGI ambapo wapo Nusu Fainali na hapo Aprili 25 watacheza na Basel ya Uswisi katika Mechi ya kwanza na kurudiana Wiki moja baadaye.


uuuuuu...

Wachezaji wa Chelsea wakionekana hoi na kama hawamo kabisa uwanjani kutetea kombe lao, labda wajaribu Europa.Demba Ba kwenye patashika uwanjani Wembley


VIKOSI:
Manchester City: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Clichy, Y Toure, Barry, Milner, Tevez (Garcia 71), Nasri (Lescott 86), Aguero
Subs not used: Hart, K Toure, Kolarov, Sinclair, Dzeko
Goals: Nasri 34, Aguero 47
Booked: Barry, Y Toure, Kompany
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Bertrand, Ramires, Mikel (Torres 65), Hazard, Mata, Oscar, Ba
Subs not used: Turnbull, Terry, Ake, Lampard, Benayoun, Moses
Goal: Ba 66
Booked: Ramires
Ref: Chris Foy (Merseyside)
Att: 85,621

No comments:

Post a Comment