MADRID, Hispania
ANDRESSA Urach (27) anaweza kuwa ndiyo sababu ya Cristiano
Ronaldo (28) kuchemka kwenye mechi dhidi ya Borussia Dortmund, baada ya Mreno
huyo kufanya ngono na Mlimbwende huyo wa Kibrazil saa 48, kabla ya mechi hiyo
ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akiwa nchini Ujerumani, Ronaldo alimsaliti mpenzi wake, Irina
Shayk na kulala na Andressa ambaye aliwahi kushiriki shindano la Miss BumBum
(Miss Wowowo) nchini Brazil.
Mwanadada huyo alifunguka kila kitu jinsi wawili hao
walivyoishia kufanya ngono hotelini, masaa 48 kabla ya Real Madrid kupigwa
mabao 4-1 na Borussia Dortmund kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Andressa alisema: “Ilikuwa raha sasa, mwili wake uko sawa,
kama miungu ya Kigiriki. Tulifanya ngono kwa muda mrefu sana na hakuacha
kusifia makalio yangu.”
Inasemekana wawili hao walianza kuwasiliana baada ya Ronaldo
kupewa namba ya Andressa na rafiki yake wa karibu mwezi uliopita, baada ya hapo
alianza kumtumia Maseji na kuwasiliana kupitia mtandao wa Skype, kabla ya
kukutana na kulala pamoja wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment