Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikocheni A Salehe Makwiro akikabidhiwa boksi lenye taa na Mkurugenzi wa Masoko wa Double Tree by Hilton, Florenso Kirambata, katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Double Tree by Hilton Sven Lippingghof.
Double Tree leo imetoa msaada wa taa zinazotumia mwanga wa jua (solar energy) kwa wanafunzi wapatao 200 wa shule ya msingi Mikocheni A jijini Dar es Salaam mradi ambao utadumu kwa miaka miwili.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye shule hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Double Tree by Hilton Sven Lippingghof alisema kuwa taa hizo zina uwezo wa kuhifadhi mwanga kwa masaa manne hivyo itamsaidia mwanafunzi kujisomea pale umeme unapokatika na vile vile ni rafiki wa mazingira tofauti na angetumia taa ya mafuta ya taa.
"Taa hizi ni za kuweka kwenye meza na ni haziharibu mazingira na afya kama ilivyo taa zinazotumia mafuta ya taa ambayo pia ni gharama kwa familia", alisema Sven
Pia halfa hiyo ilitumika kuwafundisha wanafunzi jinsi ya kutumia taa hizo ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuwasha na kuzima pia kuziongezea nguvu (recharge).
Taa hizo zinadumu kwa zaidi ya mika 10 na ukidodosha haziharibiki (hazivunjiki)
Mradi huu ulizinduliwa na mwezi uliopita na Waziri Huvisa kwenye shule ya msingi Oysterbay na utaendelea kwenye kwenye wilaya zingine za Dar esSalaam na sehemu vijijini kwenye mikoa kwa miaka miwili.
|
No comments:
Post a Comment