Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 12, 2013

WADAU WAPINGA KUONDOLEWA KWA MALINZI KWENYE KINYANGANYIRO CHA UCHAGUZI, WATISHIA KWENDA MAHAKAMANI KUSIMSMISHA UCHAGUZI WA TFF

Mdau Selemani Katto ameshangazwa na kusikitishwa na maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi kwa kumuondoa Malinzi kwa kigezo cha uzoefu.
Mdau Salum Mkemi ametoa hoja ya mwamba Malinzi ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Kagera vipi akose sifa ya kuwania nafasi ya urais wakati sifa za kuwania Urais ni zilezile. Lakini pia amekumbusha kampeni za uchaguzi wa CCM mwaka 2010 ambapo kulikuwa na bifu la Murtaza Mangungu na Juma Matandika ambaye ni ndugu yake na Malinzi hivyo wanabifu la tangu wakati huo vilevile kuna uswahiba wa tangu Temeke na Kwamba mweyekiti wa kamati ya rufaa ya uchaguzi inaongwa na Iddi Mtingijola wakati wao ni marafiki tangu ofisini wakati huo Mtingijola alikuwa bosi wa Nyamlani hivyo kuna kulindana.
Kutoka kushoto ni mdau Saidi Bakari, Ayubu Nyenzi na Dossi Matola.
Salum Mkemi akisisitiza madai yake ya kupinga maamuzi ya rufaa ya uchaguzi wa TFF.
Meza ya wadau wakipinga maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF chini ya Iddi Mtingijola.
Mdau Kaisi Edwin naye anasema kanuni mpya zimetengenezwa kwa ajili ya kuwaengua baadhi ya wagombea hivyo watasimamisha uchaguzi mahakamani na pia wanataka mahakama ya michezo CAS kuingilia kati juu ya hilo ni bora kufungiwa na FIFA. Anahoji kwa nini TFF kuna akaunti mbili jambo ambalo limemtia shaka ndio maana watu wanapingwa kuingia katika system ya mpira wa Tanzania wanaogopa maovu yatabainika.
Mdau Saidi Bakari anasema wanaamini haki iko mahakamani na sio CAS hivyo wataelekeza nguvu zao mahakamani kusimamisha uchaguzi na kwamba maamuzi ya kamati ya rufaa ya uchaguzi ni conflict of interest kwani wajumbe wengi wana unasaba na Nyamlani. Wanaanza kuanzisha matukio katika michezo ya kuanzia kesho Yanga na Lyon na Simba na Libolo ya Angola tusubiri tuone.
Mdau Ramadhani Mgeni maarufu Dogo Macho naye anasema anaamini Rais Jakaya Kikwete atasikia kilio cha wao kama wadau hivyo anamuomba aingilie kati akiwa kama kiongozi mkiubwa wa nchi.
Dada Batuli naye mdau aliyekereka na maamuzi ya kuenguliwa Jamali Malinzi.

No comments:

Post a Comment