Warembo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari leo. Mkurugenzi
wa Kampuni ya Rena Event Limited Bw Rena Calist akizungumza na
waandishi wa habari kwenye hoteli ya Seaescape iliyoko Mbezi Afrikana
jijini Dar es salaam wakati akizungumzia matayarisho ya mwisho kabla ya
shindano la Miss East Africa linalotarajiwa kufanyika kesho Desema 21
kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Katika shindano hilo wanashiriki
warembo kutoka mataifa mbalimbali ya ukanda wa nchi za Afrika Mashariki
na na baadhi ya nchi jirani na ukanda h ambapo mshindi wa shindano hilo
anatarajiwa kujinyakulia zawadi zenye thamani ya dola za Kimarekani elfu
thelathini 30,000.
Kushoto ni Guetano Kagwa ambaye
atakuwa MC wa shindano hilo na kulia ni Serge Nkurunzinza Mwakilishi wa
Miss East Africa nchini Burundi .
Guetano
Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo akizungumza na waandishi wa habari
katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kulia ni Rena
Calist Mkurugenzi wa Miss East Africa.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Warembo wanaoshiriki katika shindano hilo wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo.
Mpiga
picha wa Clouds TV Bw. Katunda akiwa katika picha ya pamoja na warembo
hao, Katunda amekuwa na warembo hao kwa muda sasa toka waingie kambini
ambapo amekuwa akichukua matukio mbalimbali katika kambi yao kwa ajili
ya kurusha kwenye kituo cha Televisheni cha Clouds.
Guetano
Kagwa ambaye ni MCwa shindano hilo na Rena Calist Mkurugenzi wa Miss
East Africa wakiwa katika picha ya pamoja na warembo hao mara baada ya
kumalizika kwa mkutano huo leo.
No comments:
Post a Comment