Wednesday, December 5, 2012
MBWANA SAMATTA KINARA WA KUFUMANIA NYAVU TP MAZEMBE MSIMU HUU
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayechezea klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta amekuwa wa kwanza katika orodha ya wafungaji bora wa klabu hiyo iliyotolewa jana.
Taarifa hiyo ambayo ipo kwenye mtandao wa klabu hiyo inasema TP Mazembe msimu wa 2012 imefunga jumla ya mabao 112 na Mbwana Samatta amefunga mabao 23.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC)humwita jina la utani Samagoal amemaliza akiwa mfungaji bora kwa kufunga mbao 23 katika mashindano yote, mabao 6 akiyafunga katika mashindano ya klabu bingwa ya Afrika ambapo alishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora wa msimu wa mashindano hayo.
Mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ameshika nafasi ya nne akiwa amefunga mabao 9 katika msimu mzima sawa na Given Singuluma.
Ifuatayo ni orodha kamili iliyotolewa na TP Mazembe kwenye mtandao wake
1.Samatta mabao 23, 2. Mputu mabao 16, 3. Lungu mabaon 13, 4.Ulimwengu na Singuluma mabao tisa, 6. Kanda na Traore mabao sita, Salakiaku mabao matano, 8. Bokanga na Kalaba mabao manne, 10.Lusadisu na Sinkala TUSILU mabao matatu, 13. Ilongo, Kasongo, Nkulukuta, Kabangu mabao mawili, 17. Hichani, Kasusula, Kanteng, Lofo, Sunzu na sundry.
Katika ligi ya mabingwa wa Afrika wanaongoza kwa mabao ni
Emmanuel CLOTTEY wa Berekum Chelsea ambaye amefunga mabao 12 matatu kwa Penati
Mbwana Samatta alifunga mabao sita ya kawaida sawa na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe Treasury Mputu lakini yeye moja ni kwa njia ya penalti na Mohamed Aboutrika wa Al Ahly lakini yeye mabao mawili ni kwanjia ya penalti.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment