Patashika
nguo kuchanika ya michuano ya Tusker Challenge cup inatarajia kuendelea
tena jioni ya leo kwa michezo miwili ya nusu fainali ya michuano
kupigwa katika dimba la Namboole nchini Uganda.
Mchezo
wa kwanza utakuwa ni baina ya timu ya taifa ya Zanzibar Zanzibar Heroes
kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars.
Katika
mchezo wa pili wenyeji Uganda Uganda Crane watakuwa wakishuka dimbani
dhidi ya Kilimanjaro Stars mchezo ambao utapigwa usiku baada ya mchezo
wa nusu fainali ya kwanza.
Timu ya
taifa ya Uganda Uganda Cranes itakuwa na kila sababu ya kutaka kutetea taji
lake hii leo kutokana na ukweli kwamba itakuwa ikicheza ikiwa katika uwanja wa
nyumbani mbali na kuwa itakuwa ikishangiliwa na mashabiki wake kibao ambao
wanaingia bure uwanjani Mandela kitongoji
cha Namboole.
Timu hizi
zimesha kutana mara tatu katika hatua kama hii ya nusu fainali baada ya
kukutana 2010 na 2011. Uganda ilishinda mwaka jana kwa mabao 3-2 mwaka jana
ilihali Kilimanjaro Stars ikishinda mwaka 2010 kwa njia ya penati 5-4.
Mpaka kufikia
hatua hii ya nusu fainali, Uganda iliiondosha Ethiopia kwa mabao 2-0 katika
robo fainali jumanne kule Namboole wakati ambapo Kilimanjaro ikiifungisha
virago Rwanda kwa ushindi kama huo jumatatu kule Lugogo.
Kocha Kim
Poulsen anatarajiwa kutokibadilisha sana kikosi chake ambapo mlinda mlango Juma
Kaseja atakuwa kiongozi wa kikosi, matarajio ni kuwa ataendelea kuwatumia
walinzi Amir Maftaha, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani na kitasa ni kama kawaida
Shomari Kapombe.
Viungo ni
Frank Dumayo, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar washambuliaji watakuwa ni Mrisho Ngasa, Simon
Msuva ambao watakuwa wakimsaidia mshambuliaji wa kati wa pekee John Boko.
Uganda Cranes
inatarajiwa kumtumia mlinda mlango Hamza Muwonge huku kocha Bobby Williamson
akitarajia kutumia ukuta wake ambao haujaruhusu bao mpaka sasa ukiongozwa na Denis
Guma na Godfrey Walusimbi upande wa pembeni na sehemu ya kati ya ulinzi
akitarajia kuwatumia Isaac Isinde na Henry Kalungi.
Viungo ni Hassan
Wasswa, Geoffrey Kizito Baba na Moses Oloya.
Williamson
bila shaka ataendele kuwatumia, Hamis Kiiza na Robert Ssentongo ambao katika
michezo miwili ya hivi karibuni walionyesha kuchangamka zaidi.
Sambamba na
hao kocha huyo anatarajia kumtumia Emmanuel Okwi ambaye amepewa kazi ya
kuwanyonga Kilimanjaro kwa kuwa anawafahamu vema akisaidiwa na Brian Umony
No comments:
Post a Comment