Balozi wa china nchini Tanzania Lu Youiquing amemkabidhi vifaa mbalimbali vya ngoma, muziki na filamu waziri wa habari,
utamaduni na michezo katika Dr Fenella Mukangara kwa lengo la kuimarisha
mahusiano katika nyanja za kitamaduni na filamu nchini.
Akiongea wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Balozi
Lu Youiquing amesema vifaa hivyo mbali na kuendeleza sekta nzima ya burudani
lakini pia vifaa hivyo vitasaidia kupunguza gharama za utayarishaji wa muziki
na uhariri wa picha za filamu kwa wadau wa tasnia hizo.
Kwa upande wake Dr Mukangara amesema wamepokea vifaa vingi
ikiwemo ngoma, magitaa na vifaa vingine ambavyo ni adimu nchini ambavyo
vitaimarisha ubora wa filamu.
Dr Fenera amesema baadhi ya vifaa vitapelekwa chuo cha sanaa na vingine vitapelekwa katika kitengo cha filamu kwa kuwa kuna baadhi ya vifaa ni kwa ajili ya kufanyia editing.
No comments:
Post a Comment