Mabao mawili ya Robert Ssentongo na moja la mshambuliaji nyota wa klabu ya Simba Emmanuel Okwi jana yamefanikisha kuwapa nafasi timu ya taifa ya Uganda “Uganda Cranes” nafasi ya kucheza fainali ya CECAFA Tusker Cup 2012 baada ya kuichapa Kilimanjaro Stars mabao 3-0 mchezo uliochezwa katika dimba la Mandela ulioko katika kitongoji cha Namboole.
The Cranes ilianza
kuandika bao la kwanza dakika ya 7 kwa bao zuri la mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Mshambuliaji
huyo wa Simba alipiga shuti mpira umbali wa mita 6 kutoka katika lango la
Kilimanjaro baada ya kupokea mpira wa kupenyezwa kutoka kwa Denis Guma .
Kipindi cha
pili Uganda Cranes iliendelea kulishambulia lango la Kilimanjaro na kutawala
mchezo na kufanikiwa kuandika bao la pili kupitia Robert Ssentongo kunako
dakika ya 53 baada ya kupokea pasi ya Godfrey Walusimbi.
Mshambuliaji
huyo wa URA aliandika bao lake la pili na la tatu kwa Uganda Cranes kunako
dakika ya 73 baada ya kumalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango Juma Kaseja uliotokana
na shuti la adhabu la Moses Oloya.
Kwa ushindi
huo wa Uganda sasa unarejesha kumbukumbu ya nyuma ya fainali ya mwaka 2008 ambapo
walikutana na wapinzani wao wakubwa katika soka la Afrika Mashariki na kati.
Kwa upande waoTimu ya
taifa ya Kenya Harambee Stars imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Cecafa
Tusker Cup 2012 baada ya kuindosha kwa mikwaju ya penati 4-2 timu ya taifa ya Zanzibar
baada ya dakika 90 za kawaida na baadaye kuongezwa dakika 30 kuhitimisha dakiak
120 za mchezo.
Ulikuwa ni
mchezo wa funga nikufunge ambapo iliwachukua Zanzibar dakika 20 kuanza kuandika
bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji Khamis Mcha Khamis kabla ya Harambee
kusawazisha dakika ya 30 kupitia kwa mlinzi nahodha Nadir ‘Cannavaro’ Haroub kuupiga
kichwa mpira baada ya krosi ya uchonganishi ya Kevin Omondi akiwa karibu na
Mike Barasa.
Zanzibar ilipata
bao la pili kupitia penati iliyopigwa dakika ya 75 na Aggrey Ambrose Morris’ penati
iliyotokana na nahodha wa Harambee Anthony Kimani kumuangusha katika eneo la
hatari mshambuliaji Juma Jaku Juma.
Dakika tano
baadaye mshambuliaji mkongwe Mike Barasa alisawazisha.
Katika hatua
ya penati wachezaji Khamis Mcha Khamis na Uthman Ali wa Zanzibar walikosa penati zao huku
Mike Barasa, Joackins Atudo, Edwin Lavasta na Abdallah Juma wakifunga penati
zao kwa upande wa Harambee licha ya Sabril Makame na Samih Nujju kufunga penati
zao haikusaidia kutinga fainali.
No comments:
Post a Comment