Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 24, 2012

AZAM BINGWA WA UHAI CUP 2012

 Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu akimkabidhi nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul Mgaya kombe la Ubingwa wa  michuano ya Uhai Cup 2012 baada ya timu hiyo kuifunga Coastal Union ya Tanga kwa penalti 3-1 katika mchezo wa fainali ya vijana chini ya miaka 20 uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 kwa sare ya mabao 2-2. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Ten.
 
 Azam FC mabingwa wapya wa Uhai Cup wamepata fedha taslimu shilingi 1.5 na Coastal Union wakiambulia shilingi million 1 kama zawadi ya washindi wa wa pili.
 (Picha na Habari Msetoto Blog)
 
SIMBA YAPATA NAFASI YA TATU
Simba imetwaa nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu zenye umri chini ya miaka 20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kuitandika Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 3-0.
Hadi mapumziko katika mechi hiyo iliyochezwa leo asubuhi (Desemba 23 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, Simba ilikuwa mbele kwa bao 1-0.
Mabao yote ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Ramadhan Mkipalamoto. Mfungaji alifunga bao la kwanza dakika ya 43 wakati mengine alipachika dakika za 57 na 70. Kwa kunyakua nafasi ya tatu, Simba imeondoka na kitita cha sh. 500,000.
Rambadhani Mkipalamoto ndiye aliyeibuka mfungaji bora wa mashindano hayo.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah akimkabidhi zawadi ya mfungaji bora wa mashindano ya vijana chini ya miaka 20 ya Uhai Cup, Ramadhani Mkipalamoto wakati wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment