WABUNIFU 23 KUTOKA TANZANIA KUONYESHA
UBUNIFU WAO
SWAHILI FASHION WEEK KUSHEHEREKEA MIAKA
MITANO
Onyesho kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati
linarajiwa kufanyika siku tatu mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia
tarehe 6, 7 na 8 Desemba, 2012 ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja
wadau 50 katika tasnia ya Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na
nyengine kuweza kuonyesha ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia
ya mitindo katika ukanda huu.
“Mwaka tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka
Tanzania wataweza kuonyesha ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya
Tanzania, ambao wote wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia
wabunifu 16 walionyesha ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion Week
yaliyofanyika Nairobi, Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa Swahili Fashion
Week, Washington Benbella
Katika kuongeza maonyesho ya mitindo, mwaka huu Swahili
Fashion Week shopping Festival ambayo ilianza 2010 itakuwepo tena kwa mara
nyengine ambapo itashirikisha zaidi ya waonyeshaji 30 katika sehemu moja ikiwa
ni kwa ajili ya kuonyesha na kuuza bidhaa za ubunifu hivyo kuifanya kuwa msimu
mkubwa manunuzi ya kazi za ubunifu wa mitindo hapa Tanzania.
Kama ilivyo ada, Swahili Fashion Week inatoa nafasi kwa
kuendeleza vipaji, ambapo tarehe 24 Novemba, 2012 kutakuwa na mchujo wa wazi kwa
wanamitindo wapya na wanaochipukia kwa jinsia zote, na mnamo tarehe 7 Desemba,
2012 kutakuwa na warsha kwa ajili ya wabunifu wote Tanzania chini wadhamini
wakuu wa warsha hiyo USAID Compete ambayo itafanyika katika Hotel ya Golden
Tulip” Aliongeza Benbella
Mashindano tofauti yamepangwa kufanyika wakati wa Swahili
Fashion Week, ikiwemo Shindano la kumtafuta Mbunifu Bora anaechipukia na Mbunifu
Bora wa kubuni Fulana. Sio tu inatoa changamoto na ari ya ushindani katika
tasnia ya ubunifu nchini Tanzania, bali pia inaweka msingi imara kwa wabunifu wa
baadae.
“Sherehe maalum za kufungua Swahili Fashion Week
zinarajiwa kufanyika siku ya Jumapili tarehe 25 Novemba, 2012, Thai Village
kuanzia saa 9 usiku. Sherehe hizo pia zitafuatiwa na kutangazwa kwa majina ya
waliochaguliwa kushindania tuzo mbalimbali zilizowekwa katika vipengele 16, tuzo
hizi ni za kwanza na ndio pekee katika ukanda huu. Tiketi za sherehe za uzinduzi
wa Swahili Fashion Week 2012 zinapatikana sehemu zifuatazo, Thai Vilage, Mgahawa
wa Epidor uliopo Masaki, na Tanzania Mitindo House” Alisema Meneja Uhusiano,
Hassan Mrope
“Tukiwa na mipango yenye ndoto za kutangaza biashara ya
mitindo katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, ninapenda kuchukua nafasi hii
kuwashukuru washirika wetu pamoja na
wadhamini wetu ambao karibia ya wote wamekuwa wakitusaidia kutokea
maonyesha yaliyopita mpaka sasa. Pia tuwashukuru sana watu wote wanaosaidia
tasnia ya mitindo hapa Tanzania kwa si tu kuhudhuria matamasha na maonyesho kama
haya bali pia kwa kununua bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini kwani hii
inatangaza kinachotengenezwa Africa “Made in Africa”. Alimalizia
Benbella
Swahili Fashion Week 2012 imedhaminiwa na Vodacom, USAID
Compete, Origin Africa, EATV, East Africa Radio, Golden Tulip Hotel. Amarula,
Precision Air, 2M Media, Global Outdoor Ltd, Vayle Springs Ltd, Eventlites,
Ultimate Security, BASATA (Baraza
La Sanaa Tanzania), Perfect
Machinery Ltd, Ndibstyles, PKF Tanzania and 361 Degrees.
KWA
MHARIRI
KUHUSU
SWAHILI FASHION WEEK
Swahili Fashion
Week ni jukwaa kubwa la mitindo ya mavazi la kila
mwaka katika ukanda wa Afrika mashariki na kati kwa sasa. Huu ni mwaka wa Tano sasa, ambapo Swahili Fashion Week
imekuwa ni Jukwaa la wanamitindo na watengeneza vito vya urembo kutoka katika
nchi zinazoongea Kiswahili na bara zima la Afrika kwa ujumla kuweza kuonesha
vipaji, kutangaza ubunifu wao na kukuza mtandao wa mawasiliano ya kibiashara
ndani na nje ya nchi kwa wadau wa mitindo. Hili limelenga kuhamasisha ukanda huu wa Afrika
Mashariki na Kati kwamba ubunifu wa
mavazi ni njia moja wapo ya kujipatia kipato na wakati huo huo kukuza bidhaa
zinazotengenezwa Afrika ( Made in Africa
concept)
Ikiwa imeanzisha uhai na jukwaa la matumaini kwa kilinge cha mitindo
katika ukanda huu, Swahili Fashion Week Swahili Fashion week imelenga kuwa
maonyesho ya ubunifu wa mavazi linaloonekana sana Afrika na hasa kwa ajili ya
soko la kimataifa, lililoundwa, kutengenezwa na kujengwa mwaka 2008 na Mustafa
Hassanali.
Ifikapo mwaka 2013, Swahili Fashion Week ina lengo
la kuwa ni tukio litakalotokea mara mbili kwa mwaka, ambapo kwa kuanza tukio la
kwanza litafanyika nchini Kenya kama sehemu ya kwanza kisha tukio lenyewe kabisa
kufanyika baadae nchini Tanzania kama sehemu ya pili.
No comments:
Post a Comment