Timu ya soka ya vijana waliochini ya miaka 17 ya Tanzania bara
Serengeti Boys jumapili itacheza dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazzaville
uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha Msaidizi wa Serengeti Boys
Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na
rufaa mkononi kutokana na kile alichokieleza kuwa wachezaji wengi wa
Congo wanaonekana kama wana umri mkubwa.
Julio
amesema amepata nafasi ya kuwaona wachezaji hao asubuhi ya leo wakati
wakifanya mazoezi na ushahidi wa machoni unaonyesha wazi kuwa wachezaji
hao wengi wao si chini ya umri wa miaka 17.
Julio
amesema ana imani kuwa wachezaji waliopimwa vipimo vya umri na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF kwa siyo hao walikokuja nchini.
Jana kocha Jacob Michelsen alisema ana
wasiwasi wa kucheza na wachezaji vijeba ambao wengine walishiriki kombe
la dunia mwaka jana na kutolewa katika hatua ya 16 bora na Uruguay,
kimsingi amesema hilo analiacha kwa shirikisho la soka TFF.
Lenzi ya Michezo imejaribu kuperuzi mtandao wa shirikisho la soka duniani FIFA ambapo imebaini wachezaji wengine ni zaidi ya umri wa miaka 17.
Katika
kikosi kilichoshiriki kombe la dunia kwa vijana nchini Mexico kuna
wachezaji 8 ambao wana umri zaidi ya miaka 17 ambao wamezaliwa si zaidi Oktoba, 1994 ambao kimsingi wamezidi umri wa miaka 17.
Wafuatao ni baadhi ya wachezaji waliozidi umri maana walishiriki kombe la dunia la vijana
1 Chill
NGAKOSSO 26/07/1994 GK 191
2 Stevy
SAMBA 03/06/1994 DF 177
3 Melvan
LEKANDZA 02/04/1994 DF 186
4 Ange
SITOU 24/05/1994 MF 176
5 Elvia
IPAMY 27/09/1994 FW 175
6 Gildas
MPASSI 10/01/1994 FW 175
7 Gloire
MAYANITH 13/10/1994 DF 181
8 Christ
NKOUNKOU 27/07/1994 FW 180
Kikosi cha Congo Brazzaville kilicho shiriki kombe la dunia mwaka jana hiki hapa
Nr. | Name | Date of Birth | Position | Height |
---|---|---|---|---|
1 | Chill NGAKOSSO | 26/07/1994 | GK | 191 |
2 | Cisse BASSOUMBA | 13/05/1996 | DF | 183 |
3 | Stevy SAMBA | 03/06/1994 | DF | 177 |
4 | Charvely MABIALA | 31/03/1996 | MF | 179 |
5 | Melvan LEKANDZA | 02/04/1994 | DF | 186 |
6 | Tierry KOUYIKOU | 17/01/1995 | MF | 177 |
7 | Ange SITOU | 24/05/1994 | MF | 176 |
8 | Hardy BINGUILA | 17/07/1996 | MF | 178 |
9 | Elvia IPAMY | 27/09/1994 | FW | 175 |
10 | Justalain KOUNKOU | 02/08/1996 | FW | 169 |
11 | Ramaric ETOU | 25/01/1995 | DF | 173 |
12 | Gildas MPASSI | 10/01/1994 | FW | 175 |
13 | Gloire MAYANITH | 13/10/1994 | DF | 181 |
14 | Christ NKOUNKOU | 27/07/1994 | FW | 180 |
17 | Bel EPAKO | 17/04/1995 | FW | 173 |
18 | Kader BIDIMBOU | 20/02/1996 | FW | 176 |
19 | Amour LOUSSOUKOU | 05/12/1996 | MF | 178 |
20 | Mavis TCHIBOTA | 07/05/1996 | FW | 177 |
21 | Pavelh NDZILA | 12/01/1995 | GK | 185 |
No comments:
Post a Comment