CHAMA cha waamuzi nchini (FRAT) kimepata viongozi wapya kupitia uchaguzi mkuu uliofanywa leo kwenye ukumbi wa CCT mjini Dodoma.
Kufuatia matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa chama hicho, Alhaj Muhidin Ndolanga alimtanga Omar Abdukadir kuwa mwenyekiti baada ya kupata kura 28 kati ya kura 29 zilizopigwa.
Wagombea wengine walikuwa ni Amry Sentimea aliyepata kura moja na Mwalimu Nassoro aliambulia patupu.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wapiga kura walikuwa 30, Juma Chaponda alipata kura 25, Tito Haule 4 na Juma Mpuya alipata kura 1
Katibu mkuu ni Charles Ndagala aliyepata kura zote 29 zilizopigwa huku akiwaacha Abdallah Mitole na Hamis Kisiwa mikono mitupu.
Jovin Ndimbo mgombea pekee wa aliutwaa nafasi ya mweka ya hazina baada ya kupata kura zote 29 zilizopigwa kwa nafasi hiyo.
Mjumbe wa mkuu mkuu wa shirikisho la soka nchini (TFF) ilikwenda kwa Sudi Abdi kura ambaye alipata kura 28 huku kura moja ikimkataa.
Wajumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni Emanuel Chaula aliyepata kura 29 na Samson Mkotya aliyepata kura 28 na Ruvu Kiwanga alikosa baada ya kupata kura sita tu.
Mwakilishi wa wanawake ilikwenda kwa Isabela Kapera aliyepata kura 29.
Akiongea kabla ya kuanza mkutano mkuu wa uchaguzi Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo Muhidin Ndolanga alisema kuwa alipigiwa simu na Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF Deus Lyato akimweleza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa kutokana na taratibu kadhaa za uchaguzi huo kutokamilika.
Kitu ambacho Ngolanga amekipinga akidai kuwa mwenye uwezo wa kuahirisha uchaguzi ni kamati ya uchaguzi ya FRAT na siyo vinginevyo.
Pia wajumbe wa mkutano huo walisikitishwa na kitendo cha Katibu wao Mkuu Lesley Liunda ambaye alikuwa anamaliza muda wake kutohudhuria mkutano huo tena bila kutoa taarifa.
No comments:
Post a Comment