Ulimwengu akipongezwa na Tusilu |
MSHAMBULIAJI chipukizi wa Kimataifa
wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),
Thomas Ulimwengu jana aliifungia timu yake mabao 3 "hat-trick" dhidi
ya 6 waliyoshinda dhidi ya Virunga katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini humo.
TP Mazembe iliandika bao la kwanza
kupitia kwa Kanda Tisuli aliyepokea pasi safi toka kwa Thomas Ulimwengu dakika
ya kwanza.
Katika dakika ya 20 Ulimwengu
aliwanyanyua mashabiki wa timu hiyo, kufunga bao baada ya kuuwahi mpira ulikuwa
unaelekea kuleta madhara langoni mwa wapinzani wao na mabeki wa Virunga
kuzembea kuokoa.
Kama vile haitoshi dakika ya 29
Super Ulimwengu kama wanavyomwita wakongo alifunga bao lingine kabla ya
kuitimisha lingine dakika ya 52.
Mshambuliaji Cheibane Traore
alifunga bao la tano dakika ya 61 na karamu ya mabao ilihitimishwa na kiungo
Mianga Ndonga
TP Mazembe wanakabiliwa na
michezo miwili ya Lupopo na DCMP na kesho wanacheza na FC Saint Eloi Lupopo,
mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Kibassa Maliba Lubumbashi na Oktoba 30,
mwaka huu watacheza na DCMotema Pembe kwenye Uwanja wa Stade des Martrs
Kinshasa.
No comments:
Post a Comment