Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 15, 2012

SIMBA YAANZA KUTETEA UBINGWA VEMA

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi  akiwa na mpira huku Jacob Masawe wa African Lyon akimfuata kwenye mechi ya ufunguzi wa ligi kuu bara, Simba imeshinda 3-0

Mshambuliaji wa Simba Daniel Akuffo akidhibitiwa vilivyo na mchezaji wa African Lyon



Amri Kiemba wa Simba akiwa na mpira huku Adam Kigwande akimkimbiza




TIMU ya Simba ya Dar es salaam imeanza vizuri kulitetea kombe lake la ligi baada ya kuifunga African Lyon bao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Mabao ya Simba yalifungwa na Emanuel Okwi, Cholo na  Daniel Akuffo ambaye alifunga kwa penati baada ya Okwi kufanyiwa fauli eneo la penati
Simba waliutawala mchezo sana hivyo matokeo waliyopata ya 3-0 walistahili sana.

Matokeo mengine ni kama ifuatavyo
Uwanja wa Sokoine Mbeya Yanga 0-0 na Prison
Uwanja wa Kaitaba Kagera Azam 1-0 Kagera Sugar bao lilifungwa na Humudu

Uwanja wa Jamhuri Morogoro Mtibwa  Sugar 0-0 Polisi Moro
Uwanja wa Chamazi Dar JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting
Uwanja wa Mkwakwani Tanga Coastal Union 1-0 JKT Mgambo
Uwanja wa CCM Kirumba Toto African   1-1     JKT Oljoro

No comments:

Post a Comment