Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 14, 2012

MISS RED'S TEMEKE SEPT 21 PTA SABASABA

MASHINDANO ya urembo Kanda ya Temeke "Redd's Miss Temeke" yanatarajiwa kufanyika Sept 21, mwaka huu katika ukumbi wa PTA (SabaSaba Hall) uliopo Temeke, jijini Dar es Salaam.

Shindano hili litashirikisha warembo 15 kutoka vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe na linatarajiwa kuwa na ushindani sana kutokana na warembo kuwa bomba.

Mkurugenzi wa BMP Promotions,Benny Kisaka ambaye ndie waandaaji wa Miss Temeke, alisema kwamba warembo hao ambao wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki mbili sasa, chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji na Dickson Daud watapanda jukwaani wanawania nafasi tatu za kupata tiketi ya kwenye shindano la taifa, Redd's Miss Tanzania itakayofanyika baadaye mwaka huu.

Pia Benny amesema shindano hilo, litakuwa na burudani ya bendi Sanjari na muongozaji maarufu katika sanaa nchini ambaye atakuwa akiongoza burudani ya mashabiki kupata kile wanachotarajia.

Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Magesse mwaka 2001, Sylvia Bahame mwaka 2003 na Genevieve Mpangala.

Amesema mbali na kinywaji cha  Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Kampuni ya gazeti la Jambo Leo, Dodoma Wine, Push Mobile, City Sports Lounge, katejoshy.blogsport.com

Wengine ni GlobalPublishers kupitia magazeti yake pendwa,100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Mariedo Boutique na 88.4 Clod's FM.

Warembo wanaendelea na mazoezi na wataongezeka wakufunzi akiwemo Miss Temeke 2002, Regina Mosha na Miss Temeke 2003 na Hawa Ismail na kutoa uzoefu wao na jinsi walivyofanikiwa katika fani hiyo na kuwapa uzoefu wao katika mashindano ya urembo

No comments:

Post a Comment