CHAMA cha waamuzi mkoa wa Dar es salaam (FRAT)juzi kilipata uongozi mpya baada ya kufanya uchaguzi mkuu kikatiba kwenye ukumbi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF)
Nafasi ya M/kiti imechukuliwa na John Ndimbo ammbaye alipata kura 6 akafuatiwa na Hamisi Kisiwa kura 3 na Lucas Agoro ambaye alikuwa anatetea nafasi yake hakupata kura.
Nafasi ya Katibu imekwenda kwa Sijali Mzeru alipata kura 6 na Abdala Mitole ambaye alikuwa anatetea nafasi yake alipata kura 3.
Katibu Msaidizi Benedicto Mtula alipata kura 6, Mjumbe wa Mkutano Mkuu ni Hemedi Nteza alipata kura 5, Mjumbe wa kamati ya utendaji ni Careson Swila ambaye naye alipata kura 5 na mwakilishi wa wanawake ni Isabela Kapera aliyejizolea kura 9 za wajumbe wote, Nafasi hizi zilikuwa na mgombea mmoja mmoja
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mkiti wa kamati ya uchaguzi Salum Matimbwa alisema uchaguzi umefanyika kwa amani na uhuru na jumla ya wajumbe tisa waliohudhuria na kupiga kura.
Pia aliwapongeza wajumbe kwa ukomavu wao walioonyesha kwani hakuna kura iliyoharibika kitu kinachodhirisha waamuzi ni wataalaum makini.
"Nawapongeza kwa uchaguzi na pia kwa umakini wenu kwani hakuna kura hata moja iliyoharibika, sababu inayonifanya niseme waamuzi ni watalaamu makini", alisema Matimbwa.
Naye Alhaj Muhidin Ndolanga ambaye ni M/Kiti wa kamati ya uchaguzi wa Chama cha waamuzi Taifa alishukuru wajumbe wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanikiwa kufanya uchaguzi na kupata uongozi mpya kwani inarahisisha kufanyika kwa uchaguzi wa FRAT Taifa.
"Kwanza nawapongeza kwa kufanya uchaguzi na kupata viongozi kwani mnaweza kafanya uchaguzi na msipate viongozi kutokana na kutopata kura zinazotosheleza toka kwa wajumbe",alisema Ndolanga.
Nao viongozi waliochaguliwa waliwashukuru wajumbe kwa imani ambayo walionyesha kwao na kuahidi kufanya kazi bega kwa bega na wanachama wote ili kukifikisha chama kwenye malengo waliojiwekea kama sera walizotoa zinavyosema.
Pia wakawataka wanachama kulipa ada mapema na kila msimu ili kukipatia chama mapato kwani hawana vyanzo mbadala vya mapato ili waweze kuendesha ofisi na na shughuli za chama za kila siku.
No comments:
Post a Comment