Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, September 10, 2012

WANARIADHA WAMWOMBEA MZEE STEVEN AKWAARE



Wanamichezo wa mashindano ya riadha yaliyofungwa jana wamesema wamesononeka kumkosa mwanariadha mkongwe mwenye historia ya pekee nchini Tanzania na duniani kote John Steven Akwaare ambaye ni mgonjwa.
Mzee Steven alilazwa siku mbili kabla mashindano ya riadha hajaanza jijini Dar es salaam baada ya kuugua ghafla kwani alianguka na kupoteza fahamu.

Akitoa salamu za pole na kukosa kumwona Mzee Steven ambaye ameshiriki mashindano ya Olympic mara saba Rais wa R.T Anthony Mtaka alisema wamesikitika kumkosa ila wanamwommbea kwa mungu apate nafauu na kuomba wanamichezo kumwombea ili apone na kurejea tena kwenye hali yake ya awali.

Pia Mtaka alisema wamezungumza naye na anaendelea vizuri kwani fahamu zimesharejea na kuwa R.T itatuma mjumbe aende kumjulia hali kwani amelazwa hospitali ya Hydom Mbulu mkoani Manyara.

Naye Benjamin Michael mshiriki pekee kutoka Kigoma alisema alitamani awaone wanariadha wenye historia ya kipekee kwenye riadha kwani na yeye ana ndoto ya kufika mbali kama wao hivyo kutomwona Mzee Steven imemsonenosha.

Benjamin ni moja ya washiriki ambaye licha kuwa ni mwanafunzi alijipia nauli kuja japo hakupa medali kwani hata vifaa hakuwa navyo sababu iliyofanya akimbie peku lakini anasema amejifunza mengi na safari ya riadha ndio imeanza

Mzee Steven anakumbukwa na wanamichezo kwa kauli yake aliyoitoa wakati alipoumia kwenye mashindano ya Olympic ya 1978 iliyofanyika Mexico na kutibiwa na kuendelea kukimbia huku anachechemea mpaka akamaliza mbio. Waandishi wahabari wakamuuliza imekuwaje ameendelea kukimbia wakati ameumia na anajua hatashinda na kusema "Sikutumwa kuanza mbio tu nilitumwa kumaliza pia"

Add caption
Mzee Steven ni miongoni wa wanamichezo ambao walionyesha moyo wa uzalendo kwa nchi yake na ndio maana kamati ya Olympic ya duniani inampa mwaliko wa kushiriki Olympic kila inapofanyika ila kumekuwepo na baadhi ya watu wanamcheleweshea mwaliko wake na muda mwingine kuacha kumpa kabisa sababu iliyofanya kamati ya Olympic ya duniani iwe ina mwalika yenyewe sasa.

No comments:

Post a Comment