TIMU ya Small Prison imeibuka bingwa wa mashindano ya Kimati Cup baada ya kuifunga Kiomoni F.C bao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa juzi kwenye uwanja wa Lamore jijini Tanga.
Akizungumza na Habari za michezo kwa njia ya simu Mratibu wa Mashindano Ibrahim Kidiwa alisema Small Prison wamekuwa mabingwa wa Kimati Cup na mshindi wa pili ni Kiomoni huku nafasi ya tatu ikienda kwa Torabora F.C
Mshindi wa kwanza Small Prison walijipatia zawadi ya jezi seti moja, mshindi wa pili Torabora aliondoka na mipira miwili wakati mshindi wa tatu Torabora alipewa mpira.
Pia alisema timu yenye nidhamu ni Mido F.C wao walizawadiwa jezi seti moja na mfungaji bora ni Peter Fear wa Torabora F.C alizawadiwa shilingi elfu 20.
Kidiwa aliwataka waandaji wengine wajitokeze kudhamini mashindano mengine ili kusaidia vijana wasijiingize kwenye makundi maovu.
"Vijana wakiwa na shughuli za kufanya hawawezi kujiingiza kwenye makundi maovu hivyo nawaomba wadhamini wajitokeze kudhamini michezo kama alivyofanya Kimati ili vijana wasijiingize kwenye makundi maovu", alisema Kidiwa.
Wakati huohuo Katibu wa chama cha waamuzi wilaya ya Tanga Ibrahim Kidiwa amewataka watu wote wanaotaka kujiunga na kozi ya uamuzi wafike kwenye ofisi za chama hicho zilizoko kwenye uwanja wa Mkwakwani leo saa 4.00 asubuhi.
Kidiwa alisema sababu iliyofanya kutoa wito huu ni kutaka kuongeza idadi ya waamuzi kwani idadi ya waamuzi inapungua kutokana kustaafu kwa mujibu wa kanuni na wengine kuhamishiwa kikazi.
Ili ujiunge na uamuzi unatakiwa uwe umemaliza kidato cha nne.
No comments:
Post a Comment