Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 27, 2012

 SAYARI YAIADHIBU UZURI 4-1, MBURAHATI YAWA BINGWA
TIMU  ya  Sayari jana iliifunga timu ya Uzuri mabao  4-1 katika mchezo wa ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam, mchezo ambao ulikuwa ni kiporo baada ya ligi kumalizika Agosti 22, mwaka huu.

Mchezo huo ulianza saa kumi jioni ulichezwa kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume, uliopo Mtaa wa Shauri moyo, Ilala ulihudhuriwa na mashabiki wachache sana ila timu zilicheza mchezo mzuri sana.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Sayari wakiongoza kwa bao moja lililofungwa na Saumu Salim baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Fatuma Bahau “Crouch”.

Baada ya mapumziko timu zote zilifanya mabadiliko ambayo hata hivyo Sayari ndio walinufaika kwani dk 48 Fatuma Mustapha alifunga bao safi baada ya kumwona golikipa wa Uzuri Anifa Idd ametoka na dakika ya 60 alifunga bao jingine na bao la nne lilifungwa na  Zaina Nassoro.

Neema Richard aliifungia Uzuri bao la  kufuta machozi baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Jamila Kassim na pengine Uzuri wajuta kukosa pointi tatu za mchezo huu kwani washambuliaji walikosa umakini katika kupiga mashuti golini.

Pamoja na Sayari kushinda mchezo huu ambao ulikuwa ni wa kiporo baada ya ratiba kumalizika Agosti 20  mwaka huu, matokeo haya hayawezi kuishusha Mburahati kileleni.

Mburahati ndio mabingwa wa ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam baada ya kufikisha pointi 28 kwenye mchezo wao wa mwisho ambao walikuwa wacheze na Sayari lakini Sayari wakaingia mitini.

Kwa  matokeo ya  jana Sayari wamefikisha pointi 24 wakiwa nafasi ya pili. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Tanzanite wenye pointi 19 na Uzuri wanashikilia nafasi ya nne wakiwa na pointi 17.

No comments:

Post a Comment