Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 27, 2012

FANYENI MAZOEZI
TIMU ya soka inayoundwa na madaktari wanaofanya kazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Muhimbili wameiasa jamii kupenda kufanya mazoezi ili kujiepusha na maradhi ambayo yamekuwa yakishambulia miili yao.

Madaktari hao ambao hufanya mazoezi kwenye uwanja wa Don Bosco Osterbay kila mwishoni mwa wiki na siku za sikukuu wamesema magonjwa mengi yanasababishwa  na staili za maisha ya kila siku na kukosa nafasi ya kushughulisha mwili ili utoke jasho.

Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO  mmoja wa madaktari hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Boaz alisema watu wamebadili sana mfumo wa maisha ambao umesababisha miili kushambuliwa na magonjwa kama ya moyo, uzito mkubwa, saratani na mengine mengi.

Pia alisema ulaji wa vyakula  vya viwandani ni hatari sana  maana wengi wanakula na huwafanyi mazoezi kitu ambacho kinapelekea ile ziada kubaki mwilini na kusababisha magonjwa, ndio maana sisi wameamua kuanzishe timu ili wafundishe jamii kwa vitendo umuhimu wa  mazoezi.

“Mazoezi ni muhimu ili kusaidia uyeyushwaji wa vitu tunavyokula vifanye kazi iliyokusudiwa ili kuepusha madhara mwilini mfano magonjwa ya moyo uzito mkubwa na mengineyo. Watu wengi tunakwenda kazini na gari, tunakula vyakula vyenye mafuta, na mwili hujaufanyi kazi yoyote.
Mwili unakuwa hatarini, hivyo tunaihasa jamii itenge muda wa kuanzia dk 20 hadi 45 kwa siku kufanya mazoezi hata kama ni kuruka kamba, kutembea kwa miguu au kukimbia mwendo mdogo au kucheza michezo mbalimbali angalau mara tatu kwa wiki hupati muda wa kufanya kila siku”, alisema Boaz

Pia alisema jamii ijitahidi kula vyakula vinavyopatikana kwenye mazingira yetu na si kununua vyakula ambayo vimetengenezwa viwandani ili kupunguza magonjwa ya unene kupita kiasi kwani unene si mzuri unasababisha magonjwa ya moyo na kisukari na hata uwezo wa kufikiri unapungua.

No comments:

Post a Comment