T IMU ya Yanga leo imeifunga African Lyon bao 4-0 kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa leo.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Didier Kavumbagu dk ya 6 baada ya shuti lake kumbabatiza beki wa African Lyon.
Bao la pili lilitiwa kimiani na Simon Msuva dk 55 na la tatu lilifungwa Haruna Niyonzima dk 57 kwa penalti baada ya Simon Msuva kufanyiwa rafu na beki Musasa Obina wa African Lyon.
Karamu ya mabao ilifungwa na Jerryson Tegete dk 88 baada kuachia shuti kati lililomshinda mlinda mlango wa lyon.
Kwa ujumla mchezo ulikuwa mzuri kwani kila timu ilicheza mchezo wa kiungwana japo Lyon ilifungwa.
|
Beki Musasa Obina wa African Lyon akipambana na mshambuliaji Luhende wa Yanga kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa leo uwanja wa Taifa |
|
|
Kiungo mshambuliaji Adam Kingwande wa African Lyon akimkimbiza Haruna Niyonzima |
|
|
Kiungo mshambuliaji wa African Lyon aliyelala akimdhibiti Niyonzima wa Yanga |
|
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la tatu alilofunga Simon Msuva |
|
|
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mpambano wao na African Lyon |
|
Yanga inaondoka kesho kwenda nchini Rwanda kwa ajili ya michezo wa kirafiki na Rayon na Polisi na itarejea nchini mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment