Rais Samia Anavyochagiza Siasa za Maridhiano na Diplomasia ya Uchumi Katika Kuijenga Tanzania
Wakati Tanzania
ikiendelea kukumbuka kipindi kigumu cha kihistoria kilichofuata kifo cha ghafla
cha Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli, mnamo Machi 19, 2021, uongozi wa
nchi umeendelea kuimarika chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia
misingi ya amani, uwezeshaji wa kidiplomasia, na mageuzi makubwa ya kiuchumi.
Kupitia mwongozo
wa wazi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Dkt. Samia
aliapishwa kuwa Rais mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi, akichukua
kijiti katika mazingira ya kipekee na kugeuza sintofahamu ya awali kuwa
matumaini mapya kwa wananchi.
Kabla ya kushika
wadhifa huo wa juu, Dkt. Samia alijijengea uzoefu mpana wa kisiasa na kiutawala
tangu kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1987, uzoefu uliomwezesha
kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya serikali na chama, pamoja na
kuwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini katika jopo la Umoja wa Mataifa
lililohusika na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.
Uzoefu huo
uliweka msingi thabiti wa mtazamo wake wa uongozi unaozingatia ushirikishwaji
na ujasiri katika kusimamia uwajibikaji wa umma, mapambano dhidi ya rushwa, na
utoaji wa haki bila kuvumilia uzembe.
Uwezo wake wa
kiuongozi ulidhihirishwa tena alipochaguliwa rasmi na wananchi kushika usukani
wa nchi katika uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya CCM, ambapo Tume Huru ya Taifa
ya Uchaguzi ilimtangaza mshindi kwa kura nyingi zilizompa mamlaka ya kuiongoza
awamu ya sita.
Chini ya uongozi
wake, Tanzania imeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta za kipaumbele zikiwemo
elimu, afya, miundombinu, na huduma za jamii, sambamba na usimamizi madhubuti
wa uteuzi wa viongozi wa kitaifa uliofanyika kwa utulivu na bila misukosuko ya
kisiasa.
Katika kujenga
mshikamano wa kitaifa, Rais Samia anatumia falsafa yake ya 4R inayojumuisha
Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi mpya wa taifa.
Hivi karibuni,
Julai 30, 2026, alifanya mazungumzo rasmi na viongozi wa vyama vya siasa katika
Ikulu ya Dar es Salaam ili kuimarisha amani na mshikamano. Juhudi hizo za siasa
za kistarabu zimekwenda sambamba na uundaji wa Tume ya Haki Jinai ili kuboresha
mifumo ya kisheria nchini.
Katika nyanja ya
kimataifa, serikali imeweka msisitizo mkubwa kwenye diplomasia ya uchumi, hatua
iliyofungua milango ya ushirikiano na taasisi za kifedha, nchi mbalimbali, na
mashirika ya kimataifa, huku Tanzania ikiendelea kuwa mwenyeji wa mikutano
mikubwa ya kimataifa na kuimarisha nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki na eneo huru la biashara barani Afrika.
Kupitia ushiriki wake katika filamu ya The
Royal Tour, utalii wa Tanzania umezidi kutangazwa duniani kote.
Sambamba na hayo,
utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati umeendelea kuleta mageuzi makubwa ya
kiuchumi, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ujenzi wa
Reli ya Kisasa (SGR), na Daraja la Kigongo-Busisi, miradi ambayo imethibitisha
utashi imara wa kisiasa katika kuleta maendeleo ya kudumu.
Ni dhahiri kwa
siaza zake za kistaarabu,uongozi wake umeendelea kuwa chachu ya usawa wa
kijinsia, ukiwahamasisha wanawake kushika nafasi za juu za maamuzi na
kuhakikisha ushiriki wao unachangia kikamilifu katika ustawi wa taifa.

Post a Comment