Rais Samia alipokutana na Rais Museveni Ikulu Dar es Salaam



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo, tarehe 06 Agosti, 2026.

Katika ziara hiyo rasmi, viongozi hao wameshuhudia utiaji saini wa Hati ya Makubaliano (MoU) inayohusu mapendekezo ya kuendeleza Tanga kama Kituo cha Nishati cha Kikanda.

Hati hiyo imesainiwa na taasisi na kampuni tatu kuu:

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) likiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Mussa Makame.

Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Bi. Proscovia Nabbanja.

Kampuni ya Biashara ya Mafuta na Nishati ya Vitol ya Bahrain ikiwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Tom Baker.

Baada ya hafla hiyo ya utiaji saini, Waziri wa Nishati wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, pamoja na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Dkt. Musenero Masanza, walizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelezea umuhimu wa makubaliano hayo kabla ya Rais Samia kuagana na mgeni wake Mhe. Rais Museveni mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo.








No comments