RAIS SAMIA AKUBALI KUJIUZULU KWA MAKAMU WA RAIS DK. NCHIMBI, TARATIBU ZA MRITHI KUCHUKULIWA



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea na kuridhia barua ya ombi la kujiuzulu kutoka kwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, tarehe 25 Agosti 2026.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka, imeelezwa kuwa kujiuzulu huko kunatarajia kuanza rasmi tarehe 04 Septemba 2026, huku taratibu za kikatiba za kupata mrithi zikifuata.

Akizungumzia uamuzi huo kupitia taarifa yake ya tarehe 25 Agosti 2026, Dkt. Nchimbi ameeleza kuwa ameamua kustaafu siasa na utumishi wa umma kwa kuzingatia Ibara ya 50(2)(c) ikisomwa pamoja na Ibara ya 149(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Aidha, Dkt. Nchimbi amemshukuru Rais Dkt. Samia na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa imani kubwa waliyonayo kwake, na ametumia nafasi hiyo kuwashukuru Watanzania wote kwa ushirikiano wao wakati wote wa utumishi wake,na kuwahakikishia kuwa ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania.

No comments