MBUNGE WA BUKOMBE DKT. BOTO BITEKO AISISITIZA AMANI NA MSHIKAMANO KWENYE MAZISHI YA DIWANI



Mbunge wa Jimbo la Bukombe na aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Doto Biteko, amewataka Watanzania kuendelea kuuenzi na kuudumisha utamaduni wa amani, upendo, umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa misingi hiyo ni nguzo muhimu ya maendeleo endelevu ya Taifa. 

Akizungumza wakati wa ibada na mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ilolangulu, Kabula Ndabacha, yaliyofanyika wilayani Mbogwe, Dkt. Biteko amesema nyakati za mafanikio na changamoto zinahitaji wananchi kuendelea kuthaminiana, kusaidiana na kuishi kwa upendo bila kujali tofauti zao, huku akisema amani ni urithi mkubwa wa Tanzania na msingi wa maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa nchini. 

Aidha, ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema kifo cha Ndabacha ni pigo kubwa kwa familia, wananchi wa Kata ya Ilolangulu na chama hicho kutokana na mchango wake katika kuwatumikia wananchi, na amehimiza jamii kuendeleza mema yote yaliyoachwa na marehemu kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kuimarisha mshikamano na kulinda amani ambayo imekuwa tunu na fahari ya Tanzania.

No comments