Kifo cha baba yake chamchanganya Messi



LIONEL Messi  amesema hana uhakika kama ataendelea kucheza soka kwa muda gani baada ya kufariki kwa baba yake. 

Baba yake, Jorge amefariki akiwa na umri wa miaka 68 wiki iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu. 

Jorge alikuwa wakala wa Messi tangu alipokuwa na umri wa miaka 14 na kushuhudia akiwa mmoja wa wachezaji wakubwa duniani. 

“Sijui nini kitaendelea kufanyika bila wewe,” aliandika katika mtandao wake wa kijamii, Messi ambaye ameshinda tuzo nane za Ballon d’Or. 

Messi aliongeza kuwa hajui jinsi ya kulichukua hilo akisema, “Kazi yangu ilikuwa ni kucheza soka tu, na sasa sina uhakika kama nitaendelea kucheza kwa muda mrefu.” 

Aliongeza; “Ulikuwa upande wangu kuanzia mwanzo. Tulikuwa karibu sana hadi mwisho, kwa nini usingesubiri kidogo tukamaliza pamoja?”.

Messi aliiongoza Argentina wakati ikitwaa Kombe la Dunia mwaka 2022 na kuiongoza tena katika fainali ya mwaka huu, ambayo timu yake ilifungwa kwa bao 1-0 na Hispania, kabla ya kurejea katika klabu ya Miami ya Marekani. 

Alirudi nyumbani na familia yake baada ya kifo cha Jorge katika Hospitali ya Rosario nchini Argentina.

 Messi alisema haamini kama baba yake amefariki dunia na ilikuwa vigumu kwake kufikiria na sasa hatamuona tena, na wala hawataongea tena.

No comments