Dolly Parton azikwa
Nguli wa muziki wa country, Dolly Parton, amezikwa kando ya mumewe, Carl Thomas Dean, katika makaburi ya Woodlawn yaliyopo Nashville, Marekani, kufuatia ibada ya faragha iliyofanyika Ijumaa, Agosti 28.
Parton alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa saratani mnamo Agosti 25.
Maziko ya msanii huyo yamethibitishwa rasmi na mpwa wake, Lainey, kupitia mtandao wa Instagram, ambapo alitoa salamu nzito za rambirambi na kueleza jinsi marehemu alivyokuwa nguzo kuu ya maisha yake na chanzo cha kumjengea kujiamini tangu utotoni.
Katika ujumbe huo uliojaa simanzi, ndugu huyo alieleza namna atakavyomkosa kuanzia kicheko chake, sauti na simu za ghafla za alfajiri kutoka kwa shangazi yake, huku akiwashukuru wote waliotuma ujumbe wa pole na maua katika kipindi kigumu cha maombolezo.

Post a Comment