WATAALAMU WAFICHUA SIRI YA MARAIS KUTEUA MAJAJI KUCHUNGUZA SKANDALI KUBWA


Uteuzi wa Majaji kuongoza tume za uchunguzi pindi nchi zinapokabiliwa na migogoro au matukio makubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu una misingi mirefu ya kisheria na kiutendaji. 

Wataalamu wa masuala ya ikulu wanaeleza kuwa misingi hii inatokana na mazoea na mifumo ya kisheria iliyopokewa kutoka katika Nchi za Jumuiya ya Madola. 

Jumuia hizi zimezoea kuwatumia majaji kama viongozi wa uchunguzi pindi inapotokea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu kama vile mauaji ya kutatanisha, mateso, au unyanyasaji wa kiwango cha juu, kwa lengo la kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana bila upendeleo.

Sababu kuu ya kuwatumia majaji inajikita katika viwango vya juu vya utendaji kazi na uzoefu mkubwa walionao watu hao katika kuhoji mashahidi, kupokea ushahidi, na kusimamia misingi ya utawala wa sheria. 

Jamii kwa asili yake ina imani kubwa na mhimili wa mahakama, na inawaona majaji kama watu huru wasioingiliwa na mamlaka za kisiasa au kiutendaji. 

Uhuru huu mkubwa wa tume za kijaji unaleta taswira ya haki mbele ya macho ya wananchi, na kuifanya taarifa au maamuzi yatakayotolewa baada ya uchunguzi kukubalika kwa urahisi kama jambo lililotendeka kwa uadilifu wa hali ya juu.

No comments