Bi. Khadija Kopa Afunguka Tetesi za Mimba ya Zuchu



Malkia wa mipasho nchini Tanzania, Bi. Khadija Kopa, amevunja ukimya na kuzitolea ufafanuzi tetesi zinazosambaa kwa kasi mtandaoni kwamba binti yake, Zuhura Othman 'Zuchu', anatarajia mtoto na bosi wa WCB, Diamond Platnumz.

Akizungumza akiwa kwenye studio za Wasafi, Khadija Kopa amewataka wadadisi wa mambo na mashabiki kuacha kumfanya yeye kuwa msemaji wa suala hilo, badala yake wawaulize wahusika wenyewe.

Khadija Kopa aliweka wazi kuwa mambo ya ujauzito ni ya kifamilia zaidi na akawanyooshea kidole waandishi kwenda moja kwa moja kwa Diamond Platnumz ambaye ndiye anayetajwa kuwa  mwenza wa Zuchu.

"Bosi wenu yuko hapa, mnapaswa kumuuliza yeye maswali hayo moja kwa moja kwa sababu bosi wenu ni mume wa Zuhura... Hayo mambo si yangu; ni ya familia yao," alisema Bi. Kopa.

Hata hivyo, nguli huyo wa Taarab hakuficha furaha yake iwapo tetesi hizo zitakuwa kweli. Alieleza hisia zake za dhati na upendo mkubwa alio nao kwa Diamond Platnumz, akisisitiza kuwa atafurahi sana kupata mjukuu kutoka kwake.

 "Mwenyezi Mungu awabariki na mtoto mwema, mwenye hekima na imani—atakayeshika dini kama wazazi wake na kuwa nguzo kwa wazee wake."

Kauli hiyo ya Khadija Kopa imeleta msisimko mkubwa mtandaoni, huku mashabiki wakigawanyika katika mitazamo tofauti:

Shabiki aliyejitakmbulisha kama Zuuh_oufit _tz alimpongeza mama huyo kwa kuonyesha upendo wa dhati kwa Diamond tangu zamani, akiona ni ndoto inayotimia. Naye Dramahq & Mama_Leylah alimpongeza Kopa kwa msimamo wake wa kutoingilia mambo ya ndani ya watu wazima, akisema ni ukomavu kutohadithia maisha ya watoto wake.

Airdanjesegaaray yeye alivutiwa na jinsi Khadija Kopa alivyo mama mkwe bora, asiye na makuu na anayependa wakwe zake.


No comments