Waamuzi 17 wapata beji za FIFA
WAAMUZI 17 wa mpira wa miguu wamepata beji za Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa (FIFA) kwa mwaka 2026.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa orodha hiyo ambapo katika orodha hiyo, waamuzi wa kati ni sita ambao ni Ahmed Arajiga, Nasir Salum, Ramadhan Kayoko, Hery Sasii, Tatu Malogo na Amina Kyando.
Waamuzi wasaidizi ni Hamdani Ally, Kassim Mpanga, Frank Komba, Mohamed Mkono, Rajabu Ramadhan, Glory Tesha, Zawadi Yusuf, Mary Seleman na Respicious Dismas ambaye amechukua beji ya Janeth Balama baada ya kufeli mtihani wa utimamu wa mwili
Pia kuna waamuzi wawili wa soka la ufukweni ambao ni Msilombo Jackson na Ally Mohamed.
Tanzania imeendelea kupata idadi hiyo kwa misimu wa tatu mfulululizo hali inayoonesha kukua kwa soka hapa nchini.

Post a Comment