Kocha wa Stellenbosch ya Afrika Kusini atua kwa Wekundu wa Msimbazi
Simba imemtambulisha Steve Barker kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo.
Barker ambaye alikuwa anaifundisha Stellenbosch ya Afrika Kusini, anachukuwa nafasi ya Dimitar Pantev aliyoondoka mapema mwezi huu, kutokana na matokeo mabovu kwenye mechi za kimataifa.
Barker (57) raia wa Afrika Kusini, aliiongoza Stellenbosch kufika nusu fainali za Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, ikitolewa na Simba ambayo iliibuka na ushindi wa jumla wa 1-0.
Msimu huu, Barker alirudi kwenye michuano hiyo akiwa na Stellenbosch na tayari alikuwa ameiongoza katika mechi mbili, akishinda 1-0 dhidi ya Otoho nyumbani na sare ya 1-1 dhidi ya Singida Black Stars ugenini.

Post a Comment