Maandamano yakosa wadau Marekani
Na Mwandishi Wetu.
Mwanaharakati wa mitandaoni, Mange Kimambi, amejikuta katika
hali ya aibu baada ya maandamano aliyoyatisha nchini Marekani tarehe 17 Oktoba
2025 kushindwa kuvutia umati kama alivyotarajia.
Licha ya kufanya kampeni kubwa kupitia mitandao ya kijamii
na kutoa ahadi kwamba Watanzania wengi wanaoishi Marekani wangekwenda kumuunga
mkono, tukio hilo lilishuhudia mahudhurio duni, hali iliyoashiria ukosefu wa
uungwaji mkono wa kweli.
Tukio hilo limebainisha ukweli kwamba sauti kubwa mtandaoni
si kigezo cha ushawishi katika uhalisia. Mange, ambaye amejitambulisha kwa muda mrefu kama msemaji wa wananchi,
inaonekana hakusoma kwa usahihi mtazamo
na hisia za Watanzania wanaoishi nje ya Nchi kuhusu ajenda zake za kisiasa na
kijamii.
Wengi wa Watanzania wanaoishi Marekani wameonekana kuchoshwa
na siasa za majukwaa ya mtandao na badala yake wanaunga mkono mabadiliko ya
kweli yanayoendelea kufanywa nchini Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa ujumla, kushindikana kwa maandamano hayo ni somo muhimu
kwa wanaharakati wote kwamba nguvu ya maneno mtandaoni haiwezi kuchukua nafasi
ya vitendo halisi.
Ni wazi kwamba watanzania wanatakiwa kutafakari kwa kina
kile kilichotokea Marekani na uhalisia wa mambo kwani wao ndiyo hasa wanaoshuhudia
maendeleo yanayoendelea kuonekana kuliko hao walioko nje ya Nchi.

Post a Comment