SHIRIKISHO
la Soka Tanzania (TFF) limesema
maandalizi ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa
Aprili 29 yanaendelea vizuri.
Akizungumza leo Ofisa habari wa TFF, Cliford Ndimbo alisema
mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa
lakini mageti yataanza kufunguliwa saa 2:00 asubuhi
“Jeshi la
polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limesema ulinzi wa kutosha na kutoa
tahadhari kwa wote wenye nia ya kufanya vitendo vya uovu,” alisema Ndimbo
Pia Ndimbo
alisema mamlaka ya uwanja imethibitisha kuongezeka kwa camera ambapo sasa
zimefikia 109 na zitakuwa zinafuatilia matukio yote ndani ya uwanja na kuwataka
mashabiki wasiwe na hofu kwani kutakuwa na huduma ya vyakula na vinywaji ndani.
Aidha
alisema tiketi zinaendelea
kuuzwa kupitia Selcom na unatakiwa kujaza pesa kwenye kadi yako ya Selcom
ambayo itakuweza kununua tiketi kupitia simu ya mkononi.
Viingilio
katika mchezo huo ni Sh 30,000 kwa
VIP A, VIP B na C ni Sh 20, 000 huku Mzunguko ikiwa ni Sh 7000 tu.
No comments:
Post a Comment