USHINDI wa
michezo miwili katika wiki ya 11 ya Ligi ya mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es
Salaam (RBA) umetosha kuiweka kileleni Oilers kwa kufikisha pointi 26 katika
michezo 13 iliyocheza.
Oilers iliifunga
Kigamboni kwa vikapu 129-67 na Ukonga kwa vikapu 62-55 katika michezo
iliyochezwa katika viwanja vya Bandari, Kurasini.
Savio
inashika nafasi ya pili baada ya ushindi wa vikapu 58-44 dhidi ya ABC na
kujikusanyia pointi 21 katika michezo 11 iliyocheza sawa na Vijana ambayo
iliifunga Kurasini Heat kwa vikapu 90-56 ambayo imecheza michezo 12.
Pazi ambayo
iliifunga UDSM insiders kwa vikapu 66-47 inashika nafasi ya nne baada ya
kufikisha pointi 19 sawa na JKT ambayo iliifunga Mabibo kwa vikapu 62-51 na
Magnet 96-69.
Ukonga kings
inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 19 baada ya kuifunga Mabibo kwa vikapu
43-39, ABC na Mabibo baada ya kufungwa zimebaki na pointi 18 na Mannet licha ya
kufungwa na Tanzania Prisons kwa vikapu 68-57 imebaki kwenye nafasi ya
tisa ikiwa na pointi 16.
Jogoo
inashika nafasi ya 11 licha ya kufungwa na UDSM Insiders kwa vikapu 73-70 na Kigamboni
licha ya kufungwa na Magone ambayo inaburuza mkia kwa vikapu 45-47.
Kwa upande
wa wanawake JKT Stars baada ya kuifunga Ukonga Queens kwa vikapu 42-31 inaongoza
ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza michezo sita na kufungwa mmoja.
Ukonga
Queens inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tisa, DonBosco Lionesses
inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi saba, Vijana, Jeshi Stars na Oilers
Princesses zina pointi tano.
No comments:
Post a Comment