TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys imefanikitwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Challenge U-17 baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Somalia kwenye Uwanja wa Ngozi mjini Bujumbura, Burundi.
Ushindi huo umetokana na mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66 katika mchezo ambao Serengeti Boys ilionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafurahisha mashabiki.
Ikumbukwe Somalia imefika
hatua hii baada ya kuwatoa Uganda, wakati Tanzania iliwatoa Kenya katika mechi
za nusu fainali. Ushindi huo umetokana na mabao ya Edson Jeremiah dakika ya 25 na Jaffar Mtoo dakika ta 66 katika mchezo ambao Serengeti Boys ilionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwafurahisha mashabiki.
Katika fainali hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad alikuwepo na kukabidhi Kombe kwa mabingwa, ambao msafara wao uliongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia
No comments:
Post a Comment