WAWAKILISHI
wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika, Yanga, wamejiweka katika nafasi
ngumu ya kufuzu kucheza hatua ya makundi baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Township
Rollers ya Botswana katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es
Salaam.
Kwa matokeo hayo, mabingwa hao wa Tanzania
Bara, sasa wanahitaji ushindi wa kuanzia angalau mabao 2-0 na kuendelea.
Katika
mchezo wa jana wageni waliandika bao la kwanza katika dakika ya 11 kupitia kwa Lemponye
Tshireletso aliifungia bao Township Rollers bao la kuongoza baada ya kupiga
shuti kali nje ya meta 18 lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Obrey Chirwa
aliisawazishia Yanga katika dakika ya 30 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa
Tshishimbi.
Yanga
walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini wachezaji wake hawakuwa makini
na kukosa mabao.
Katika
dakika ya tatu, wapinzani wa Yanga nusura wafunge baada ya Joel Morogorosi
kutokuwa makini na mpira kuwahiwa na kipa wa Yanga, Ramadhani Kabwili.
Ibrahim Ajib
alikosa bao katika dakika ya 25 baada ya kupiga mpira uliopaa juu ya lango la
wapinzani wao hao kutoka Botswana.
Yanga
ilianza kwa nguvu kipindi cha pili kwa kufanya mashambulizi kadhaa, ambapo
katika dakika ya 48 nusura wapate bao
baada ya Gadiel Michael kushindwa kufunga kwa kupiga shuti kali lililopaa juu
ya lango.
Timu hizo
zitarudiana mjini Gaborone, Botswana Machi 17 katika mchezo wa utakaoamua timu
ipi itinge hatua ya makundi huku Yanga ikiwa na kibarua kigumu zaidi.
Nahodha wa
Yanga, Pius Buswita akizungumza baada ya mchezo huo jana, alisema kuwa
wapinzani wao walitumia vizuri nafasi walizopata, lakini na wao wanaweza
kushinda katika mchezo huo wa ugenini.
Kikosi
cha Yanga: Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Said Ali,
Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Pius Buswita, Pato Ngonyani, Ibrahim Ajibu/Juma
Mahadhi, Obrey Chirwa na Emmanuel Martine/Mwashiuya.
No comments:
Post a Comment