TIMU ya
taifa ya Tanzania kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro
Heroes, leo imeshindwa kutumia uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa
suluhu dhidi na wenzao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika
pambano hilo la kusaka kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika
zitakazofanyika mwakani Niger, Ngorongoro Heroes pamoja na kupata kona
nyingi, ilishindwa kabisa kuzifumania
nyavu za wapinzani wao hao kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo
hayo, Ngorongoro Heroes sasa inahitaji sare ya kuanzia angalau bao 1-1 au
ushindi wa aina yoyote ili kusonga mbele, hatua ambayo itakutana na Mali katika
mbio za kusaka kucheza fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Kocha wa
Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje amesema kuwa ataongeza dozi kwa wachezaji wake
ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wa marudiano nchini Congo.
Naye Nahodha
wa timu hiyo, Said Bakari alisema kuwa walipata nafasi nyingi lakini bahati
mbaya walishindwa kuzitendea haki, lakini mchezo ujao watajitahidi kuhakikisha
wanaibuka na ushindi na kusonga mbele hatua inayofuata.
Ngorongoro
walipata kona 11 dhidi ya tatu za Congo, ambazo hazikuwasaidia kuibuka japo na
ushindi kiduchu.
Katika
dakika 45 za kwanza, timu zote ziliweza kutengeneza nafasi, lakini zilishindwa
kupata mabao na hivyo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana.
Kikosi cha Ngorongoro Heroes: Ramadhani Kabwili, Kibwana shomary,
Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Ally Ngazi, Assadi Juma, Kelvin
Naftai, Paul Peter/Riphat Msuya, Abdul Seleman na Said Bakari/Mohamed Mussa.
No comments:
Post a Comment