Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava (kushoto) akiwa na mgeni rasmi Fesail Asas wakimkabidhi kombe nahodha wa timu ya Iringa United baada ya kuwafunga Mtwivila City kwa penalti baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa wamefungana bao 1-1
Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na
mgeni rasmi wa fainali ya ligi ya mkoa Fesail Asas wakimkabidhi zawadi ya jezi
kampteni wa timu ya Mtwivila baada ya kuwafungwa na timu ya Iringa United kwa
njia ya mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika tisini wakiwa
wamefungana bao 1-1
Mashabiki na viongozi wa timu ya Iringa United wakishangilia ushindi baada ya kuwafunga timu ngumu ya Mtwivila City kwa njia ya mikuju ya penati na kuwa wawakilishi wa mkoa wa Iringa kwenye ligi ya mabingwa wa mikoa
TIMU ya Soka
ya Iringa United imetwaa ubingwa wa ligi ya daraja la tatu Mkoa wa Iringa baada
ya kuibuka na ushindi penalti 3-1 dhidi ya Mtwivila FC.
Katika
mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Samora
juzi timu ya Mtwivila FC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya nane
lililofungwa na mshambuliaji David Mwanga kwa uzembe wa golikipa wa Iringa
United Nelly Mkakilwa kumpita tobo.
Mchezo huo
uliokuwa wa kukamiana lakini baadhi ya wachezaji wakionyesha ufundi katika
kucheza mpira, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Mtwivila walikuwa
wakiongoza kwa bao 1-0.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi, kila timu ikionyesha haijabahatisha kufika fainali huku
Mtwivila wakitaka kuongeza na Iringa wakitaka kusawazisha.
Mchezaji wa
Iringa, Razack Kibuga aliibuka shujaa baada ya kusawazisha bao katika dakika ya
76 na kuwaacha wachezaji wa Mtwivila wakilaumiana baada ya dakika 90 kumalizika
ndipo wakapigiana penalti na Iringa ikashinda penalti 3-1 za Mtwivila
Kutokana na
ushindi huo timu ya Iringa United ilijinyakulia kikombe, jezi seti moja na
mipira miwili na timu ya Mtwivila waliondoka na jezi na mpira mmoja.
Mchezaji
bora ni Razack Kibuga wa Iringa United aliondoka na zawadi ya sh.100,000 na
cheti golikipa bora alikuwa Nelly Mkakilwa toka Iringa United aliyepata sh.50,000
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na timu ya Mkimbizi FC baada ya kuifunga timu ya Mshindo FC
kwa mabao 5-4.
No comments:
Post a Comment