MAKOCHA wa
kozi ya grassroot wametakiwa kutumia vema elimu wanayopata kuendeleza vipaji
vya soka Mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo
yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
Almasi Kasongo alipokuwa akifungua kozi ya grassroot ya makocha wa soka inayoendeshwa
na chama hicho.
“Mkoa wa Dar
es Salaam tumepanga kuhakikisha tunaendeleza mpira kwa kuendesha kozi
mbalimbali kwa makocha, waamuzi na uongozi hivyo kwa kuanza tumeanza na kozi ya
grassroot hivyo ninyoi mliopata fursa hii mhakikishe mnakwenda kutumia elemu
hiyo,” alisema Kasongo.
Pia Kasongo
alisema baada ya kozi ya grassroot itafuatia kozi ya waamuzi ambayo itahusisha
waamuzi vijana.
Kasongo
alimshukuru mkufunzi Sunday Kayuni kwa kukubali kufundisha makocha hao 25 ambao
watakuwa darasani kwa siku tano.
Kozi hiyo
inafanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam ilianza juzi na inatarajiwa
kumalizika Jumamosi.
No comments:
Post a Comment