TIMU 15
zimefuzu katika hatua ya 16 ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports
Federation Cup – ASFC katika michezo iliyochezwa Januari 30-31 katika viwanja
tofauti.
Akizungumza
jana Ofisa Habari wa Shrikisho la Soka Tanzania, Clinford Ndimbo alisema timu 10
ni za Ligi Kuu, nne ni za ligi daraja la kwanza na moja ni ya mabingwa wa
mikoa.
“Mpaka sasa
ni timu 15 zilizofuzu hatua ya 16 bora hivyo timu moja itapatikana baadae maana
mchezo huo itahusisha timu za daraja la kwanza ambazo ziliomba mechi zao
zisogezwe mbele ili wamalize ligi daraja la kwanza,” alisema Ndimbo.
Ndimbo alisema
mchezo huo utazihusisha KMC dhidi ya Toto Africans na utachezwa Februari 7 baada
ya kuhitimishwa ligi daraja la kwanza ambayo itafikia tamati Februari 4.
Timu
zilizofuzu ni Azam FC, Yanga,
Mbao FC, Ndanda FC, Tanzania Prisons, Njombe Mji, Mtibwa Sugar, Stand United, Majimaji
na Singida United.
Nyingine ni Dodoma
FC, JKT Tanzania, Polisi Tanzania, Kiluvya na mabingwa wa mkoa Buseresere
FC.
Bingwa wa
mashindano hayo anawakilisha nchi katika mashindano ya klabu bingwa barani
Afrika na mwaka huu mwakilishi ni Simba ambaye aliondolewa katika hatua ya 64.
No comments:
Post a Comment