TIMU za
Coastal Union ya Tanga na KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana zilikata
tiketi ya kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao kutoka katika Kundi B baada
ya kushinda mechi zao za mwisho.
Coastal
Union imerejea katika ligi hiyo baada ya kuifunga Mawenzi 2-0 katika mchezo
uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa, huku KMC ikiibuka na ushindi
wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mlale kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Kwa matokeo
hayo, KMC inaongoza kundi hilo kwa kuwa na pointi 28 ikifuatiwa na Coastal
Union yenye alama 26, huku JKT Mlale wakibaki na pointi zao 25 na Polisi Dar es
Salaam wameshuka daraja baada ya kumaliza wakiwa na pointi tano tu.
Katika
mchezo huo, Coastal Union waliandika bao la kwanza katika dakika ya 24
lililofungwa kwa penalti na Raizin Hafidh baada ya kuchezewa rafu.
Hatahivyo,
mashabiki wa Mawenzi waliwarushia mawe wachezaji wa Coastal Union wakati
wakishangilia bao hilo na kuzua mtafaruku.
Ulinzi
uliimarishwa baada ya vurugu hizo kufuatia kuongezwa kwa askari wa Kikosi cha
Kuzuia Ghasia, FFU.
Ukongwe wa
Athuman Idd Chuji pamoja na kipa Hussein Sharifu au Cassilas waliibeba timu yao
kutokana na uzoefu wao.
Dakika ya 72 ya mchezo huo, Chuji aliipatia Coastal
Union bao la pili lililoihakikishia ushindi timu hiyo na kuondoka na pointi
tatu muhimu.
Chuji
alifunga bao hilo baada ya kucheza kwa utulivu zaidi baada ya kupata mpira
uliopigwa na Andrew Simchimbi na kuokolewa na mabeki wa Mawenzi na kumkuta
mfungaji aliyeujaza wavuni.
Mashabiki wa
timu hiyo walikuwa wakimshangilia Chuji kwa kumuita `Babu, Babu, Babu’.
Katika
matokeo mengine ya kundi hilo, Polisi Tanzania ilibuka na ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Mufundi huku Mbeya Kwanza wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi
ya Polisi Dar es Salaam.
Timu hizo
mbili zinaungana na JKT Tanzania iliyokuwa ya kwanza kupanda daraja kutoka
katika Kundi A huku mechi za kundi hilo zikitarajia kumalizika Jumatatu huku
zile za Kundi C zitaisha kesho Jumapili.
No comments:
Post a Comment