KITENDAWILI
cha timu zitakazopanda ligi kuu msimu ujao kutoka Kundi B kinatarajiwa
kutenguliwa leo kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja tofauti.
Michezo yote
ya kundi hili inatarajiwa kuanza saa 10:00 kamili ioni kukwepa upangaji wa matokeo.
Coastal
Union watakuwa ugenini katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kucheza na Mawenzi Market, mchezo ambao ni
muhimu kwa Coastal yenye pointi 23 kushinda ili wapande daraja.
Vinara JKT
Mlale itakuwa nyumbani kuikabili KMC kwenye uwanja wa Majimaji Songea,
kwasababu timu hizi zina pointi 25 kila moja inahitaji kushinda ili ipande ila
endapo zitatoka sare na Coastal kushinda basi JKT itapanda kutokana na uwiano
mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Coastal ili
kujiweka pazuri inatakiwa kushinda kwa idadi ya mabao matatu ili kujihakikishia
nafasi moja endapo JKT na KMC watatoka sare JKT na Coastal zitapanda kwa sababu
zina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa na KMC italazimika kusubiri
msimu ujao.
Michezo
mingine katika kundi hili Mufindi itaikaribisha Polisi Tanzania yenye pointi 19
ambayo inashika nafasi ya nne na Mbeya Kwanza itakuwa nyumbani kuikabili Polisi
Dar es Salaam ambayo imeshashuka daraja.
Msimamo wa hili JKT Mlale inaongoza ikiwa na
pointi 25 sawa na KMC lakini zikiwa zimetofautiana katika mabao ya kufunga na
kufungwa, Coastal Union ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23, Polisi Tanzania
ina pointi 21, Mbeya Kwanza pointi 19, Mufindi United ina pointi 13, Mawenzi
Market ina pointi 8 na Polisi Dar es salaam pointi 5.
Michezo ya kundi
A inatarajiwa kuchezwa Februari 5 na kundi C itacheza Februari 4.
No comments:
Post a Comment