SIMBA leo imezidi kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya
kuishindilia Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa
Uhuru Dar es Salaam.
Kipigo hicho
kimeifanya Shooting kuchapwa jumla ya mabao 10-0 msimu huu, baada ya kukubali
kufungwa mabao 7-0 katika raundi ya kwanza mwaka jana.
Mabao
yaliyofungwa na nahodha John Bocco na Mzamiru Yassin yalitosha kuifanya Simba
iendelee kutamba kileleni kusaka ubingwa wa ligi ilioukosa kwa tarkiban miaka
mitano.
Bocco
anayeonekana kujijengea ufalme Simba baada ya kufanya hivyo Azam misimu kadhaa
iliyopita, aliiandikia Simba bao la kuongoza katika dakika ya 22 akiunganisha
kona iliyochongwa na Shizza Kichuya.
Katika
dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza, mpira ulilazimika kusimama baada ya
kuzimia kwa mshambuliaji mkongwe wa Simba, Emmanuel Okwi aliyefanyiwa madhambi
na beki Mau Bofu wa Ruvu ambapo alimpiga shingoni.
Rafu hiyo
ilifanya mwamuzi Hance Mabena wa Tanga kumwonyesha kadi nyekundu mchezaji huyo
wa Ruvu.
Kutoka na
rafu aliyofanyiwa, Okwi hakuendelea na mchezo na hivyo nafasi yake kuchukuliwa
na Laudit Mavugo.
Dakika ya
66, Mzamiru aliiandikia Simba bao la pili akiunganisha pasi ya Kichuya kabla
Bocco hajaifungia timu yake bao la tatu katika dakika ya 75.
Bocco
alifunga bao hilo baada ya kuwavisha kanzu mabeki na kipa wa Ruvu kabla ya kuujaza mpira wavuni.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi
38 juu ya Azam iliyo nafasi ya pili ikiwa na pointi 33 huku Yanga ikishika
nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31. Simba itacheza mechi inayofuata dhidi ya
Azam
No comments:
Post a Comment