OBREY Chirwa ameendelea kuing’arisha Yanga baada ya kuifungia mabao matatu katika
ushindi wa 4-0 dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Katika mechi
hiyo ya raundi ya pili ya Ligi Kuu, Yanga ilitawala kila idara hasa katika
kipindi cha pili baada ya Njombe kucheza pungufu kutokana na kipa wake Rajabu
Mbululo kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kudaka mpira nje ya eneo lake.
Baada ya
kwenda mapumziko kila upande ukiwa hauna bao, ilimchukua Chirwa dakika mbili
baada ya kipindi cha pili kuiandikia Yanga bao la kuongoza.
Chirwa
alifunga bao hilo akiunganisha pasi ya winga ya kulia kutoka kwa Pius Buswita.
Dakika ya 65
Chirwa alifunga bao kwa mkwaju wa penalti
iliyotolewa na mwamuzi Hance Mabena wa Tanga baada ya beki wa Njombe
kuunawa mpira eneo la hatari kabla ya Emmanuel Martin hajaifungia bao la tatu
dakika nne baadae akimalizia mpira wa Juma Mahadhi.
Zikiwa
zimesalia dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Chirwa aliandika bao la
nne akiunganisha pasi kutoka kwa Baruan Akilimali.
Matokeo hayo
yameifanya Yanga kufikisha pointi 34 nyuma ya Azam yenye pointi 31 na Simba
yenye pointi 38.
Simba
inakutana na Azam leo katika mechi yenye presha kubwa kwani kila moja inawania
ushindi ili ijisogeze ilipo.
No comments:
Post a Comment